LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAZISHI YA ALIYEKUWA RAIS WA ZANZIBAR MZEE ABOUD JUMBE KUFANYIKA LEO.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na BMG kwa msaa wa Mtandao
Mazishi ya aliyekuwa  Rais  wa pili wa Zanzibar na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mzee Aboud Jumbe, yanatarajia kufanyika leo mchana nyumbani kwake Migombani mjini Zanzibar.

Taarifa iliyotolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk.Ali Mohamed Shein, imeeleza kuwa mazishi hayo ya mzee Jumbe aliyeafriki dunia jana nyumbani kwake Kigamboni jijini Dar es salaam, yatafanyika baada ya sala itakayofanyika kwenye msikiti wa Mshawar mjini Unguja

Katika taarifa hiyo, Dkt Shein amesema enzi za uhai wake marehemu mzee Jumbe, alitoa mchango mkubwa katika kuitumikia, kuiongoza na kuijenga Zanzibar pamoja na nafasi yake katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kutokana na msiba huo Dk.Shein ametangaza siku saba za maombolezo, kuanzia leo ambapo katika kipindi hicho chote bendera zote zitapepea nusu mlingoti.

Wakati huohuo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein kufuatia kifo cha mzee Jumbe.

Katika salamu hizo Rais Magufuli amesema Taifa limempoteza mtu muhimu ambaye alijitoa kupigania Uhuru, Umoja, Haki na Maendeleo ya Wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla katika kipindi kigumu ambacho Taifa lilikipitia.

No comments:

Powered by Blogger.