LIVE STREAM ADS

Header Ads

MKUU WA MKOA WA MWANZA ATAKA WAFANYABIASHARA KUCHANGAMKIA FURSA ZA SOKO LA PAMOJA LA AFRIKA MASHARIKI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Judith Ferdinand, Mwanza
Wafanyabiashara kutoka nchi za Afrika Mashariki, wameombwa kuchangamkia fursa za kibiashara na uwekezaji zilizopo katika soko la pamoja sambamba na maonyesho mbalimbali ya ukanda huu.

Wito huo umetolewa jana na Mkuu wa wilaya ya Ilemela Dkt.Leonard Masale (pichani) aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella katika hafla ya ufunguzi wa maonyesho ya 11 ya kibiashara Afrika Mashariki yanayoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara na Wenye Viwanda na kilimo (TCCIA) Mwanza yanayofanyika kwenye uwanja wa Rock City Mall mkoani hapa.

Masale alisema, soko hilo lenye watu wapatao milioni 140,likitumika vizuri litatoa fursa ya kuuziana bidhaa wenyewe na kuleta tija kwa wateja badala ya kutegemea masoko ya nje ambayo kuyafikia yanahitaji gharama zaidi sambamba na kuimarisha mahusiano ya kibiashara kwa kubadilishana ujuzi,uzoefu na mazingira ya biashara.

Pia alisema,kupitia maonyesho hayo wafanyabiashara wa ukanda huu wanapata fursa ya kuimarisha bidhaa na huduma katika soko hilo.

Hata hivyo aliwaomba wananchi wa  ukanda huu,kuwa soko la pamoja la Afrika Mashariki limeishaanza, hivyo ni jukumu lao kuchangamkia fursa hiyo ambayo inapanua wigo wa kufanyabiashara, uwekezaji na ajira katika nchi zao.

Aidha aliitaka TCCIA kuongeza bidii  katika kutangaza maonyesho hayo, ili kuvutia makampuni zaidi kutoka nchi za ukanda huo pamoja na kuyafanya kuwa endelevu na bora zaidi.

Kwa upande wake Mwenyekiti Wa TCCIA Mkoa wa Mwanza Elibariki Mmari alisema, kupitia maonyesho hayo wajasiriamali wamepata uwezo wa kujiamini na kuzalisha bidhaa bora zitakazokubalika katika soko la pamoja.

Vilevile alisema mpaka sasa maonyesho  yepiga hatua kwa kupata uwanja unaoendana na hadhi ya Afrika Mashariki sambamba na kuongeza idadi ya washiriki 80 mwaka 2006 wakati yameanza mpaka 320 mwaka 2015.

Kadhalika aliwaomba wajasiriamali na makampuni kujitokeza kushiriki katika maonyesho hayo, kwani yamawapa fursa ya kukuza,kuboresha biashara,kujitangaza na kupata masoko.
Bonyeza HAPA Kutazama Picha

No comments:

Powered by Blogger.