LIVE STREAM ADS

Header Ads

MKUU WA MKOA WA MWANZA AZINDUA MPANGO MAALUMU WA KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI JIJINI MWANZA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella, akizungumza na watumishi mbalimbali wa halmashauri ya Jiji la Mwanza katika uzinduzi wa mpango maalumu wa kushughulikia migogoro ya ardhi Jijini Mwanza.
Na Vesterjtz

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mhe.Merry Tesha, akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo ambao umelenga kumaliza matatizo na migogoro ya ardhi Jijini Mwanza.
Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kiburwa, akizungumza katika uzinduzi huo.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, amezindua  mpango maalumu wa kushughulikia migogoro na kero za ardhi Jijini Mwanza huku akiwaagiza wakuu wa idara kutenga kila siku ya jumanne kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi kuhusu migogoro ya ardhi.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya kuwepo na migogoro ya ardhi isiyo malizika kutokana na utata wa umiliki wa ardhi (hatimiliki) kwa wananchi wa mkoa wa Mwanza hali iliyosababaisha wakazi wengi kupelekea malalamiko yao katika ofisi za mkuu wa mkoa na wakuu wa wilaya.

"Katika malalamiko kumi sita ni ya ardhi, hivyo wakuu wa idara watatakiwa kufunga ofisi na kutafuta eneo ili kuwasikiliza na kushughulikia migogoro hiyo kabla ya kuwajibishwa wenyewe,"Alisema Mongella.

Aidha Mongell aliwataka wananchi kuepuka tabia za utapeli wa kugushi nyaraka za umiliki wa ardhi na atakaye kuwa na nyaraka  bandia atafikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.
Uzinduzi wa mkakati huo ulifanyika katika viwanja vya hamashauri ya jiji la Mwanza na kuhudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Merry Tesha, Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kiburwa, pamoja na viongozi mbalimbali wa halmashauri ya Jiji la Mwanza.

No comments:

Powered by Blogger.