BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI NACTE LAKUNJUA MAKUCHA YAKE.
Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Na James Salvatory, Dar es salaam.
Baraza la Taifa la ELimu ya Ufundi nchini (NACTE) limevifutia usajili vyuo vitano huku vyuo 41
vinavyotoa elimu ya ufundi bila kusajiliwa vikipewa wiki mbili ya kujisajili wakati vyuo 175 nchini vikishushwa hadhi.
Mwenyekiti wa (NACTE), Mhandisi Steven Mlote, amesema
baraza limekuwa likivitembelea vyuo na
kubaini mapungufu ambapo kuna vyuo vimekeua namna ya utoaji wa masoma ya vyuo
hivyo.
"Kuna vyuo mchana ni chuo usiku
ni bar, na kuna vyuo vinatoa mafunzo tofauti na usajili wao na kuna vyuo
ambavyo havijasajiliwa na vinatoa mafunzo huku kukiwa kuna vyuo ambavyo muda wake umeisha wa
usajili na havijaenda kubadilisha au kuongeza hadhi yake huku kukiwa na vyuo
ambavyo havina waalimu wanaotambulika yaan wenye vibali."Amesema
Mlote.
Baraza limetoa muda wa mwezi
mmoja kwa vyuo 112 kutekeleza marsharti ya usajili na vyuo 52 kutekeleza
masharti ya ithibati kwa mujibu wa sheria za uendeshaji vyuo vya ufundi nchini na vyuo vitakavyoshindwa kutekeleza agizo hilo vitafungiwa mara moja.
Mlote amewataka
wazazi waache kuwapeleka watoto wao kwenye
vyuo ambavyo havina usajili kutoka Nacte na kama wanataka kupata vyuo ambavyo
vimetimiza masharti yote watembelee tovuti ya Nacte au wafike ofisini jijini Dar es salaam na Mikoani na wanafunzi waliokuwa wanasoma
vyuo vilivyofungiwa kuwasiliana na baraza kwa ajili ya kuwatafutia vyuo
vilivyokamilisha usajiri.
Vyuo vitano vilivyofungiwa
na Nacte ni State College of Health and Allied Sciences, Zoom Polytechnic College, Tabitha College, Financial Training Center pamoja na TMBI College of Business and Finance vyote vya Dar es salaam.
No comments: