LIVE STREAM ADS

Header Ads

MTANDAO WA KUPINGA NDOA ZA UTOTONI WASHITUSHWA NA RUFAA KUHUSU KESI YA NDOA ZA WATOTO.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Na James Salvatory, Dar es salaam
Mtandao wa mashirika yanayopinga ndoa za utotoni nchini umeitaka ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali kuondoa kusudio la kukata rufaa juu ya kesi ya kupinga ndoa za utotoni iliyotolewa hukumu kuitaka serikali kuondoa baadhi ya vifungu vya sheria ya ndoa ambavyo vinaruhusu mtoto wa kike kuolewa akiwa na umri chini ya miaka 18.

Mwenyekiti wa Mtandao huo Valeria Msoka, amesema mtandao huo ulishitushwa na taarifa iliyotolewa na mwanasheria mkuu wa serikali kuwa serikali ilikata rufaa ili kupinga maamuzi Yaliyo tolewa na mahakama kuu kwenye kesi hiyo.

Ameongeza kuwa kitendo cha Mwanasheria mkuu kukata rufaa kina ashiria kuwa serikali inaunaunga mkono ndoa za utotoni
jambo ambalo lipo kinyumena na mkataba wa kikanda na kimataifa wa kulinda haki na ustawi wa mtoto wa kike ulio sainiwa mwaka 1989.

Kwa upande wake mwakilishi wa kulinda utu wa mtoto Koshuma Mtegeti aliitaja Mikoa ya Tabora na Mwanza kuwa ni miongoni mwa mikoa inayol1ongoza kwa ndoa za utotoni.

Mapema mwezi uliopita mahakama mkuu ya Tanzania ilitoa hukumu dhidi ya kesi ya kupinga vifungu vya sheria vinavyo ruhusu
mtoto wa kike kuolewa akiwa na umri chini ya miaka 18 iliyofunguliwa na mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya Msichana Initiative dhidi ya mwanasheria mkuu wa Serikali.
Bonyeza HAPA Kusoma Zaidi.

No comments:

Powered by Blogger.