LIVE STREAM ADS

Header Ads

RAIS MAGUFULI AWASILI MKOANI MWANZA KWA ZIARA YA KIKAZI, ATOA MAAGIZO KWA HALMASHAURI ZOTE NCHINI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Rais Dkt.John Joseph Pombe Magufuli.

Judith Ferdinand, Mwanza
Halmashauri zote nchi zimetakiwa kubadilisha sheria zake ndogondogo ikiwemo za ukusanyaji ushuru na kodi kwa wakulima na wafanyabiashara wadongo kwani sheria hizo zimeonekana kuwa mizigo kwao.

Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli, ametoa agizo hilo mapema hii leo wakati akiwahutubia wakazi wa Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja Mnadani wilayani humo.

Dkt.Magufuli amesema, anataka ajenge nidhamu ya wakulima kufanya kazi pamoja na kuishi maisha mazuri, hivyo halmashauri ziache kuwatoza ushuru na kodi na badala yake ziwatoze wafanyabiashara wakubwa wakubwa.

"Nahitaji kukusanya mapato, ila siyo kwa watu maskini, nataka nijenge nidhamu kwa wakulima kufanya kazi kwa bidii, ili waishi maisha mazuri, hivyo halmashauri zote zisiwatoze ushuru na badala yake zikatafute ushuru kwa wafanyabiashara wakubwa," alisema Dkt. Magufuli.

Hata hivyo  aliwaomba, wakulima na wananchi kujikita katika kilimo ili wapate mazao ya chakula na biashara, kwani serikali ya awamu ya tano haiko tayari kuwapa chakula wale watakaokumbwa na baa la njaa.

"Serikali hii ya Magufuli haiko tayari kuwapa watu chakula na badala yake ipo kwa ajili ya kulipia wanafunzi ada ya shule ili wasome bure pamoja na kuharakisha huduma mbalimbali za maendeleo". Amesema Dkt.Magufuli.
Bonyeza HAPA kusoma ziara za JPM mkoani Mwanza!

No comments:

Powered by Blogger.