LIVE STREAM ADS

Header Ads

RAIS MAGUFULI KURINDIMA MKOANI MWANZA KUANZIA LEO.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa Mkoa wa Mwaza, Mhe.John Mongella, akitoa taarifa ya ujio wa Rais Magufuli mkoani Mwanza.
Na BMG
Leo jumatano agosti 10,2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli, anatarajiwa kuwasili mkoani Mwanza kwa ajili ya ziara fupi ya kikazi akitokea mkoani Geita alikokuwa pia na ziara pamoja na mapumziko mafupi.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, jana alisema hiyo itakuwa ni ziara fupi ya kiserikali ambapo Rais Magufuli atakuwa akizungumza na wananchi kuhusu yale ambayo amepanga kuyafanya katika uongozi wake tangu achaguliwe kuwa rais.

Alisema majira ya asubuhi hii leo, Rais Magufuli atapokelewa katika Wilayani Sengerema ambapo atasalimiana na wananchi wilayani humo na baadae kuwasili Jijini Mwanza ambap atakuwa na mapumziko Ikulu ndogo.

Kesho agost 11, Rais Magufuli anatarajiwa kufanya ziara ya kukagua na kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa daraja la watembea kwa miguu lililobo Furahisha Jijini Mwanza pamoja na upanuzi wa barabara ya Furahisha hadi Pasiansi.

Baada ya ziara hiyo, kuanzia majira ya saa nane mchana, Rais Magufuli anatarajiwa kufanya mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza ambapo atazungumza na wananchi.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (kulia) akitoa taarifa ya ujio wa Rais Magufuli mkoani Mwanza. Kushoto ni Katibu Tawala mkoani Mwanza, CP Clodwig Mtweve.
Wanahabari wakinasa matukio
Wanahabari
Bonyeza HAPA Kusoma Zaidi.

No comments:

Powered by Blogger.