TAMASHA LA KUSAKA VIPAJI VYA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI KUFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM.
Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Picha kutoka Maktaba ya BMG
Na James Salvatory, Dar es Salaaam
Tamasha la kusaka vipaji kwa waimbaji wa nyimbo za injili, bongoflava na hiphop linatarajia kufanyika mwezi ujao Jijini Dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, mkurugenzi mtendaji wa Mpea Tanzania Ltd, Stephen Hiza, alisema tamasha hilo lina lengo la kuibua vipaji vipya na kuwatengenezea ajira vijana ambao wana vipaji hivyo.
Aidha alisema kuwa tamasha hilo litakalofanyika katika chuo cha uandishi wa habari, Royal kilichopo ubungo urafiki Jijini Dar es salaam.
Alibainisha kuwa fomu za ushiriki zinapatikana chuoni hapa kwa gharama ya shilingi elfu 10,000 tu. Aidha aliwataka vijana kujitokeza kwa wingi ili kupata fursa hiyo adimu.
No comments: