LIVE STREAM ADS

Header Ads

UCHOCHEZI WAVITIA MASHAKANI VITUO VIWILI VYA REDIO NCHINI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na James Salvatory-BMG Dar
Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo imevifungia kwa muda usiojulikana vituo vya radio 5 cha Arusha
pamoja na kituo cha Redio cha Magic Fm cha jijini Dar es Salaam kwa kile kinachodaiwa vituo hivyo kurusha vipindi vyenye uchochezi.

Waziri Nape Moses Nnauye ametangaza kuvifungia vituo hivyo vya redio wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Amesema kwa mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 28(1) cha sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzannia (TCRA) ya mwaka 2003 imempa mamlaka ya kuvifungia vituo hivyo Uamunuzi wa kuvifungia vituo umefikia baada kujiridhisha kuwa Redio five katika kipindi cha matukio kilichorushwa tarehe 25 Agosti,2016 muda wa saa 2:00 usiku hadi saa 3;00 usiku ambapo katika kipindi hicho alihojiwa Mbunge wa Arusha Majini,Godbless Lema ambapo alikuwa anatoa maneno ya uchochezi.

Aidha alisema licha ya Mbunge huyo kutoa lugha hizo,lakini watangazaji wa kipindi hicho walishindwa kumsahihisha jambo analodai linakwenda kinyume na sheria ya utangazaji.

Mbali na Redio5 pia ametaja kosa lilipelekea kukifungia kituo cha Magic Fm cha Dar es Salaam, amedai mnamo tarehe 17,Agosti 2016 katika kipindi cha Morning Magic kipindi hicho kilichoruka saa 1.00 asubuhi na saa 2.30 katika kipengele cha Kupanga Rangi watangazaji wa kipindi hicho walisikika wakitoa maneno anayoeleza kuwa ni ya uchochezi.

“Watangazaji wa Magic walisema kama Rais anavunja Katiba sasa wananchi wa chini wafanyeje, nao lazima watafanya hivyo,”Alisema waziri Nape.

Amesema baada ya kuvifungia vituo hivyo kwa mda ambayo hajautaja, ameitaka kamati ya Maudhui ya (TCRA) kukutana ili waziite pande zote mbili za redio hizo ili waweze kujitetea na kamati hiyo ikishakutana na kusikiliza utetezi wa redio hizo, basi yeye atachukua hatua ya kuvifungulia au kuendelea kuvifungia.

Kufungiwa vituo hivyo inakuwa ni mwendelezo wa Waziri huyo kuvifungia vyombo vya habari ambapo kwa kipindi cha miezi nane cha Nape awe waziri katika wizara baada ya kuanza kuyafungia magazeti ya Mawio, Mseto yote yanayomiliwa na Mbunge wa Ubungo,Saed Kubenea kwa hoja kuwa yanaaandika habari za Uchochezi.

No comments:

Powered by Blogger.