LIVE STREAM ADS

Header Ads

UMATI YAWASIHI AKINA MAMA WAJAWAZITO KUONANA NA WATAALAMU WA AFYA KABLA NA BAADA YA KUJIFUNGUA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Image result for MJAMZITOJudith Ferdinand, Mwanza
Akina mama wajawazito  wameshauriwa kuwaona wataalamu wa afya kabla na baada ya kujifungua, ili kupata  elimu juu ya lishe bora inayomsaidia mama mjamzito ikiwa hana  uwezo wa kuzalisha  maziwa ya kutosha kwa ajili ya kunyonyeshea mtoto.

Ushauri huo ulitolewa  juzi na Mtaalamu wa Afya ya Uzazi  wa Kituo cha Afya  cha UMATI kilichopo wilayani Ilemela  jijini Mwanza, Jasinta  Mutakyawa,  alisema wakina mama  wengi  hawana elimu  ya juu ya  kuwapatia watoto lishe  bora,  pindi wanapotoka kujifungua, hali inayosababisha   kuzorota kwa afya ya  mtoto.

Mutakyawa  alisema,  mama  aliyejifungua na hana  uwezo  wa  kutengeza maziwa  ya kutosha  ndani ya  kifua chake, ipo lishe mbadala  ambayo anatakiwa  kumpa mtoto wake, itakayomsaidia mtoto katika ukuaji   na  kuwa na afya bora.

Pia aliwaomba, wakina mama    kuhudhuria mara kwa mara katika vituo vya afya, kwa ajili ya  kupata elimu ya malezi kwa watoto ambao wanahitaji matunzo yaliyo bora sambamba na kupunguza tatizo la  utapia mlo.

“Nawaomba  wakina mama kabla na baada ya kujifungua na   wahudhurie katika vituo vya afya (kiniki)  ili waweze kupata elimu ya  lishe bora kwa watoto kwani baadhi yao wanadhani  wakishajifua, wanakuwa wamemaliza kila kitu na,”alisema Mutakyawa

Aidha  aliwaomba  wajawazito      kuhudhuria kiliniki  kwani ni muhimu, kwa kuelimishwa juu ya mama na  mtoto ikiwemo kubaini  dalili za hatari zinazowanyemelea watoto wachanga zinazoweza kuzoofisha afya zao pamoja na ukuaji bora.

Hata hivyo aliwaomba wataalamu afya  kujitokeza kuwahudumia wa kina mama wanaofika kiliniki pamoja na  kuwapatia elimu na ushauri, kwa ajili ya kuwajengea uwezo  utakaowasaidia kugundua dalili za hatari wakati wa ujauzito ili kupunguza vifo vya mama na mtoto.

No comments:

Powered by Blogger.