LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAZIRI WA AFYA AYAGEUKIA MAKAMPUNI YA SIGARA NCHINI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com


Na James Salvatory, BMG Dar
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, ameyataka makampuni ya sigara nchini kuweka tangazo lenye maandishi makubwa linalotoa tahadhari kwa watumiaji wa bidhaa hiyo.

Mwalimu amesema hadi kufikia Oktoba Mosi mwaka huu, kila kampuni inapaswa kuweka maandishi ya "Onyo, Sigara Inaua" na kwamba kampuni itakashindwa kufanya hivyo itachukuliwa hatua za kisheria.

Aidha waziri Ummy amesema kuna mpango wa kuongeza bei ya sigara kwa lengo la kupunguza utumiaji wake huku tahadhari uvutaji sigara katika maeneo ya wazi ikitakiwa kuchukuliwa ikiwemo kuweka mabango ya kuzuia uvutaji hadharani.

Mkurugezi mtendaji wa  Chama cha kuthibiti tumbaku Tanzania, Lutgard Kokulinda, amesema ni jukumu la serikali inalinda afya kwa wananchi wake huku akitaka kilimo cha tumbaku kutopewa kipaumbele na badala yake akulima walime mazao mbadala.

No comments:

Powered by Blogger.