LIVE STREAM ADS

Header Ads

YANGA YAITISHA MKUTANO MKUU WA WANACHAMA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Time ya soka ya Yanga ya Jijini Dar es salaam imetangaza kufanya mkutano mkuu wa wanachama agost 06,2016.

Taarifa iliyotolewa leo na Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit, imeeza kwamba mkutano huo utafanyika katika ukumbi wa Police Officers Mess Jijini Dar es salaam kuanzia saa tatu asubuhi.

Taarifa hiyo imeongeza kwamba, siku hiyo pia kuanzia majira ya saa kumi jioni kutakuwa na mchezo wa kirafiki kati ya Yanga na Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro.

Japo ajenda za mkutano huo hazijawekwa wazi licha ya wanachama wa Yanga kutakiwa kuhudhuria bila kukosa, lakini BMG tunawatakia mkutano mwema wanayanga.

No comments:

Powered by Blogger.