LIVE STREAM ADS

Header Ads

MOODEWJI AANZA KUIPIGA MSASA KLABU YA SOKA YA SIMBA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Mfanyabiashara maarufu nchini Mohamed Dewji (kushoto), anaemiliki Kampuni za Mohamed Interprises Tanzania Limited (MeTL), leo ameikabidhi klabu ya soka ya Simba kitita cha shilingi Milioni 100 kwa ajili ya klabu hiyo kukamilisha usajili wa wachezaji wake.

Inaelezwa kwamba hatua hiyo imefikiwa baada ya uongozi wa Simba kumuandikia Moodewji barua ya kumuomba msaada wa fedha hizo licha ya kuwepo taarifa kwamba Moodewji aliwahi kuahidi kutoa kiasi hicho cha fedha ikiwa wanachama wa Simba watakubali kumuuzia hisa za kuimiliki timu hiyo.

Juzi jumapili Klabu ya Simba ilifanya mkutano mkuu ambao pamoja na ajenda nyingine, suala la Mo kuinunua Simba lilikuwa miongoni mwa ajenda zilizostahili kujadiliwa ambapo hata hivyo mkutano huo uliahilishwa kabla ya ajenda ajenda zote hazijajadiliwa.

Uongozi wa Simba jana jumatatu ulitoa taarifa za kukutana na Mo ili kuzungumza nae zaidi juu ya nia yake ya kuinunua klabu ya Simba kwa kiasi cha shilingi Bilioni 20 kwa kipindi cha miaka minne ambapo ataifanya bajeti ya timu hiyo kupanda na kufikia bilioni tano kwa kila mwaka.

Imeandaliwa na BMG kwa msaada wa mtandao.

No comments:

Powered by Blogger.