LIVE STREAM ADS

Header Ads

BENKI YA NMB YASHIRIKIANA NA SHULEDIRECT KUTOA ELIMU YA KIFEDHA KWA WANAFUNZI WA SEKONDARI NCHINI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na James Salvatory, BMG Dar
Benki ya NMB ikishirikiana na mkakati wa ShuleDirect wameanzisha mpango mpya wa kuwapa elimu wanafunzi wa sekondari elimu kuhusu masuala ya kifedha.

Akizungumzia mpango huo, Meneja Huduma za ziada wa Benki ya NMB, Stephen Adili, alisema NMB imeamua kushirikiana na ShuleDirect ili kuwawezesha wanafunzi kuwa na uelewa kuhusu matumizi sahihi ya fedha na kuelimiswa faida za kutunza fedha.

Aidha alisema wanataka taifa la watu wenye nidhamu ya fedha na kupitia mpango huu tutaweza kupata watanzania ambao watakuwa wanawajibika kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya taifa kwa kujua matumizi sahihi ya fedha na hata kuwa walipa kodi wazuri.

Naye Mkurugenzi wa ShuleDirect, Faraja Nyarandu, alisema pamoja na kupewa elimu lakini pia mpango huo utawasaidia wanafunzi hao kufikia malengo waliyojiwekea kimaisha kwa kuanza kuweka akiba mapema ambayo watakuwa wakiitumia hata kwa miaka ya baadae.

“Wanafunzi hawa kama wakianza kutunza pesa mapema wanaweza kuwa na mipango mizuri ya baadae, ni lazima kila kijana awajibike kwa kulisaidia taifa kupata maendeleo na maandalizi ni sasa,” alisema Nyarandu.

Kwa upande wa mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde, aliipongeza NMB na ShuleDirect
kwa kuja na mpango huo na kuwataka wanafunzi kuutumia vyema ili uweze kuwasaidia na kuwaandaa kwa maisha ya baadae.

“Jambo la nidhamu ya fedha linawashinda watu wengi, na waliofanikiwa wote lazima wawe na nidhamu ya fedha, kama vijana bado wana mambo mengi ya kufanya na elimu watakayopata kuhusu nidhamu ya fedha ni hakika itawasaidia kufikia ndoto zenu.

No comments:

Powered by Blogger.