LIVE STREAM ADS

Header Ads

BUNGE LATAKIWA KUTOPITISHA MSWADA WA MABADILIKO YA SHERIA YA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII INAYOZUIA FAO LA KUJITOA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na James Salvatory Bmg-Dar
Vyama vya wafanyakazi nchini, Asasi za kiraia pamoja na
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Bindamu nchini (THRDC), vimelitaka bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutopitisha mswada wa mabadiliko ya sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii unaokwenda kuzuia fao la kujitoa.

Hayo yalisemwa jana Jijini Dar es Salaam na Gratius Mkoba ambaye ni Rais wa Chama cha wafanyakzi nchini (TUCTA) na Rais wa chama cha Walimu nchini (CWT).

Viongozi wengine waliounga mkono tamko hilo ni pamoja Nicomemas Kajungu ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Migodini nchini (NUMET), Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakzi wa Viwandani nchini (TUICO) na Onesmo Olengurumwa, Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za binadamu nchini (THRDC).

Walisema kama wabunge wakikaidi na kuupitisha mswaada huo na baadae kuwa sheria basi wafanyakazi nchini watagoma ikiwemo kwenda mahakamani kupinga mswaada huo pamoja na kujitoa kwenye mifuko yote ya hifadhi ya jamii kutokana na mswaada huo kumkandamiza mfanyakazi nchini.

"Tunawaomba wabunge walioangalie hili, ni vigumu sana kuingia kichwani kama leo hii tumefikia hatua ya kutaka mtu anayeacha kazi akiwa na miaka 25 au 30, akae hadi kufikia miaka 60 ndipo achukue pesa zake sawa na yule aliyefanya kazi kwa kipindi cha miaka 60 na kustaafu, hapa inaonekana wameshindwa kuelewa dhana dhima matumuzi ya pesheni, kwani lengo lake ni kumsaidia mfanyakazi kazi ili maisha yaendelee vyema anapostaafu". Alimesema Mkoba.

Naye Kajungu alisema mswaada huo utawaumiza zaidi wafanyakazi wa migodi amabo wengi wao wanafanya kazi kwa mikataba kwani wanaomiliki migodi hupewa mikataba ya miaka michache hivyo nao inawalazimu kuwaajiri wachimbaji kwa mikataba mifupi mifupi.

No comments:

Powered by Blogger.