LIVE STREAM ADS

Header Ads

CHANZO CHA BODABODA KUPATA VIFO NA VILEMA VYA MAISHA CHATAJWA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Image result for bodaboda imageNa Shaban Njia, Kahama
Imeelezwa kwamba Madereva pikipiki (Bodaboda) wengi hapa nchini wamekuwa wakipata vilema vya maisha kutokana na kutofuata sheria za usalama barabara wakiwa katika shughuli zao za kutafuta riziki.

Hayo yalibainishwa juzi na Mkufunzi kutoka chuo cha ufundi cha Kingwande cha Jijijini Mwanza, Ndege Masara, katika semina ya siku nne iliyojumisha madareva pikipki iliyofanyika Mjini hapa chini ya udhamini wa Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini Jumanne Kishimba.

Masara alisema kuwa Madereva pikipiki hao wamekuwa hawapo makini wakatika wakiwa barabarani hali ambayo imefanya kuongezeka kwa ajili za Pikipiki na kuwasababishia kuwa na vilema vya maisha pamoja na abiria wanaowabeba.

Mkufunzi huyo aliendelea kusema kuwa kwa sasa Bodaboda hao wanapaswa kuwa makini wanapokuwa barabarani ikiwea ni pamoja na kutambua nini cha kufanya katika kazi yao hiyo ya ueneshaji wa vyombo hivyo vya moto na kuweza kupunguza ajali.

Pia aliwataka kutumia mafunzo hayo ya siku nne wanayoyapata katika kufuata sheria za barabarani hali ambayo italeta mabadiliko mabubwa ikiwa ni pamoja na kuacha kuapkiza abiria wawili wawili katika pikipiki moja hali ambayo inakuwa ni rahisi katika kusababisha ajali.

Hata hivyo Mkufunzi huyo aliwataka bodaboda hao kuwa na utaratibu wa kujiwekea akiba  kutokana na kazi hiyo  ikiwa ni pamoja na kusomesha watoto wao ili kuleta mabadiliko chanya katika familia wanazotoka pamoja na watu wanaowategemea.

Kwa upande wake Koplo Daudi Lugora kutoka katika kitengo cha usalama Barabarani Mjini Kahama aliwataka madereva hao kuzingatia masomo wanayoyapata kutoka kwa Mkufunzi hiyo ikiwa pamoja na kuwahamasisha wenzao kujitokeza katika kupata mafunzo hayo na kuweza kupata vyeti vitakavyopelea wao kuwa rahisi kupata leseni.

Koplo Daudi alisisiza kwa madereva hao kuacha tabia ya kunywa pombe wakati wakiendesha Pikipiki ili kuweza kupunguza ajali ambazo sio lazima ambazo zinaweza kutokea kutokana na kutumia vilevi hivyo.

Mafunzo hayo ya Madereva Pikipiki yalijumuisha washirikia zaidi ya 200 ambapo mafunzo hayo yalidhaminiwa na mbunge wa Jimbo la Kahama Jumanne Kishimba kwa lengo la kukuza Wajasiliamali wadogowadogo waliopo katika Mji wa Kahama hususani madereva wa bodaboda.

Kwa upande upande wake Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini Abdul Mpei akiongea kwa niaba ya Mbunge huyo alisema kuwa kwa sasa Vijana lazima wabadilike kwa kufanya kazi kwa kufuata sheria za nchi ikiwa ni sambamba na kupata leseni ili waweze kuwa huru katika biasahara zao.

No comments:

Powered by Blogger.