LIVE STREAM ADS

Header Ads

IDADI YA MAUZO KATIKA SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM YASHUKA KWA KASI YA JABU.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com


Na James Salvatory, BMG Dar
Idadi ya mauzo  katika  Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) imeshuka kwa asilimia 81 kutoka bilioni 9 na kufikia 1.7 bilioni katika kipindi cha wiki moja iliyopita.

Hayo yalisemwa na Afisa Masoko Mwandamizi wa DSE,
Marry Kinabo wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam na kuongeza kwamba idadi ya mauzo imeshuka kwa
asilimia 81 kutoka bilioni 9 na kufikia 1.7 bilioni, huku idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa zikishuka kwa asilimia 68 kutoka milioni 1 hadi 340,000

"Ukubwa wa mtaji wa soko umeshuka kwa asilimia 2.79 kutoka trilioni 21 na kufikia 20.7 trilioni,Ukubwa wa mtaji wa makampuni ya ndani umebaki kwenye kiwango kilekile cha Panda 8.2 trilioni. Kampuni tatu zilizoongoza kwa idadi ya hisa  zilizouzwa na kununuliwa katika kipindi cha wiki iliyopita kuwa ni benki ya CRDB kwa asilimia 53, kampuni ya bia TBL asilimia 35, na kampuni ya Swissport kwa asilimia" Alisema kinabo.

Aidha kinabo ameongeza kuwa sekta ya viwanda wiki iliyoisha imeshuka kwa alama 36.6 baada ya bei za hisa za TBL kushuka kwa asilimia 1.08. Sekta ya huduma za kibenki na kifedha imepanda kwa pointi 3.64 baada ya bei kupanda kwenye kaunta za DSE kwa asilimia 11.57 huku sekta ya huduma za kibiashara kwa wiki iliyopita imeshuka kwa pointi 4.19 baada
ya bei kupanda kwenye kaunta za Swissport.

No comments:

Powered by Blogger.