LIVE STREAM ADS

Header Ads

KAMPUNI YA TIGO YAIPIGA TAFU SERIKALI MKOANI TANGA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Mkurugenzi wa Kampuni ya Tigo Kanda ya Pwani, Goodluck Charles akiongea jana na wanafunzi wa shule ya msingi Mabawa mkoani Tanga, kwenye hafla ya kukabidhi madawati yaliyotolerwa na kampuni hiyo.

Kushoto kwake ni mkuu wa wilaya ya Tanga, Thobias Mwilapwa, Katibu tawala wilaya ya Tanga Bi. Faidha Salim na kushoto ni Meneja wa Tigo mkoani Tanga, Patricia Sempinge.
Na Krantz Mwantepele
Katibu tawala wilaya ya Tanga Bi. Faidha Salim akiongea jana na wanahabari na wanafunzi ya shule ya msingi Mabawa, kwenye hafla ya kukabidhi madawati.

Kulia kwake ni mkuu wa wilaya ya Tanga Mhe. Thobias Mwilapwa, Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Pwani, Goodluck Charles na Meneja wa Tigo mkoani Tanga Patricia Sempinge. Na kushoto kwake mwalimu mkuu Zuwena Msembo.
Mkuu wa wilaya ya Tanga Mhe. Thobias Mwilapwa (kulia)akipokea  dawati toka kwa mkurugenzi wa Tigo kanda ya Pwani, Goodluck Charles(kushoto).

Katikati ni mwalimu mkuu wa shule ya mabawa, Zuwena Msembo, Jumla ya madawati 435 yenye thamani ya shilingi milioni 72  yalitolewa na kampuni ya Tigo mkoani Tanga kwenye hafla iliyofanyika shule ya msingi Mabawa.
Mkuu wa wilaya ya Tanga Mhe. Thobias Mwilapwa (kulia) akiwa ameketi na mkurugenzi wa Tigo kanda ya Pwani(mwenye miwani) na wanafunzi  Amir Kibwana na Pili Ali(kushoto) wa shule ya msingi Mabawa, mara baada ya kampuni ya Tigo kukabidhiwa  435 yenye thamani ya shilingi milioni 72 kwa mkoa wa Tanga.
Wanafunzi wa shule ya msingi Mabawa mkoani Tanga wakiwa wameketi kwenye madawati .waliyokabidhiwa na kampuni ya Tigo.

No comments:

Powered by Blogger.