LIVE STREAM ADS

Header Ads

KATIBU WA CHAMA CHA WATU WENYE UALIBINO WILAYA YA NZEGA MKOANI TABORA ATEKWA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na George Binagi-GB Pazzo
Katibu wa Chama cha watu wenye ualibino Wilaya ya Nzega mkoani Tabora, Juma Moshi Juma, amenusurika kuuawa na watu wasiofahamika ambao wanasadikika kutaka kumkata viuongo vya mwili wake kwa ajili ya shughuli za kishirikina.

Tukio hilo limetokea jana majira ya saa nne usiku wakati katibu huyo anarejea nyumbani akitokea kwenye shughuli zake ambapo watu wawili waliokuwa na silaha za jadi walimvamia na kuanza kumcharanga mapanga.

Akizungumza na Lake Fm ya Jijini Mwanza, Katibu huyo amesema watu hao walimjeruhi kwa kumkata na panga sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo mikono ambapo alifanya juhudi za kujiokoa kwa kupambana nao huku akipiga kelele za kuomba msaada kwa majirani hali iliyosaidia wavamizi hao kutokomea kusikojulikana.

Tukio hilo limeripotiwa katika kituo cha polisi wilayani nzega na polisi wanaendelea na upelelezi ili kubaini waliohusika kwa ajili ya hatua za kisheria ambapo katibu huyo ameruhusiwa kutoka hospitali ya wilaya ya Nzega alikopelekwa kwa ajili matibabu.

No comments:

Powered by Blogger.