LIVE STREAM ADS

Header Ads

KONGAMANO LA KUHAMASISHA NA KUKUZA UWEKEZAJI KUFANYIKA MKOANI MOROGORO.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Displaying IMG_20160927_125451.jpg
Na James Salvatory, BMG Dar
Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC)kwa kushirikiana uongozi wa mkoa wa Morogoro kinatarajia kufanya kongamano maalum la kuhamasisha na kukuza uwekezaji na biashara katika mkoa huo .

Akizungumza na waandishi wa habari mapema wiki hii Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa kituo hicho Clifford Tandari amesema kuwa kongamano hilo linatarajiwa kufanyika september 29 na 30 katika hoteli Glonency iliyopo katika mkoa wa morogoro .

Aidha alisema kuwa kongamano hili linalenga kukuza sekta mbambli za viwanda ,kilimo nausindikaji wa mazao, nishati
elimu na maji pamoja na ujenzi wa majengo na sekta nyinginezo ikiwemo chakula dawa na utafiti ,usafirishaji, fedha na biashara
linatarajiwa kuhudhuliwa na waziri Waviwanda na biashara Charles Mwijage.

Kongamano hilo litaisaidia kuuweka mkoa wa Morogoro kuwa
mkoa wenye fursa mbalimbali ikiwemo kilimo na biashara kwa makampuni ya nje na ndani kuja kuwekeza katika sekta hizo.

"Jumla ya miradi 198 imekuwa ikitelezwa katika mkoa huo ambapo miradi hiyo inatarajia kuzalisha ajira 28,944 ambapo miradi 111
ni ya watanzania huku miradi 46 ni ya wageni kutoka nje," alisema

No comments:

Powered by Blogger.