LIVE STREAM ADS

Header Ads

KUMEKUCHA KIKOSI CHA SOKA CHA VIJANA NCHINI SERENGETI BOYS.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
img_3395
Timu ya Serengeti Boys ya vijana chini ya umri wa miaka 17 imepata ushindi wa mabai 3-2 dhidi ya Congo Brazzaville katika hatua ya tatu kuwania kufuzu michuano ya Afrika kwa vijana itakayofanyika mwakani AFCON 2017 Madagascar.

Magoli ya Serengeti Boys yalifungwa na Yohana Mkomola aliyefunga mawili na Issa Makamba, wakati magoli ya Congo yalifungwa na Langa Percy kwa mkwaju wa penati na Bopoumela Chardon.

Mgeni rasmi alikuwa ni Nape Nnauye ambaye ni waziri wa utamaduni na michezo aliahidi pia kununua bao moja kwa Sh 500,000 na atalipa fedha hizo kadiri ya idadi ya mabao hata kama yatafika 10 hivyo gharama yake itakuwa Sh 5,000,000. Kuna wabunge na viongozi wengine waliahidi kutoa fedha zaidi.

Timu hizo zinatarajiwa kurudiana Oktoba 2 ambapo mshindi wa hapo atasonga mbele kwa kufuzu moja kwa moja katika michuano hiyo ya vijana.

No comments:

Powered by Blogger.