LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAMLAKA YA HALI YA HEWA NCHINI YATOA TAHADHARI KWA WAKULIMA NA WAFUGAJI KUTOKANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Image result for AGNES KIJAZINa James Salvatory - BMG Dar
Imeelezwa kuwa kuna uwezekano mkubwa wa uhaba wa mvua na mtawanyiko hafifu katika kipindi cha msimu wa mvua  wa oktoba hadi disemba 2016 katika maeneo ya pwani ya kaskazini pamoja na yale ya nyanda za juu kaskazini mashariki yanatarajiwa kuwa na vipindi vingi vijkavu.

Mkurugezi wa mamlaka ya hali ya hewa nchini, Dr.Agnes Kijazi, amesema kuwepo kwa kiwango kidogo cha mvua nchini kinasababisha na hali ya joto la juu ya wastani iliyopo katika mwa  eneo la kiikweta la bahari ya pasifiki na magharibi mwa bahari ya hindi (pwani ya afrika mashariki) inatarajiwa kuendelea katika kipindi  cha Oktoba – Disemba 2016 ambapo  katika eneo la mashariki  mwa bahari ya hindi hali ya joto la juu ya wastani iliyopo inatarajiwa kuendelea katika kipindi cha  msimu  wa vuli.

Aidha Kijazi amesema kuwa hali hiyo ya mfumo wa joto inaashiria kuwepo kwa upepo wenye unyevunyevu hafifu kutoka mashariki kuelekea pwani ya Afrika Mashariki na kuongezea kwa joto katika eneo la kusini–mashariki mwa bahari ya Atlantiki karibu na pwani ya Angola hususani katika miezi ya octoba na disemba, 2016.

 Hali hiyo inaweza kunasababisha kuwepo kwa upepo wenye unyevunyevu hafifu kutoka katika misitu ya Kongo na kuelekea katika maeneo ya magharibi na katikati mwa nchi na hivyo kusababisha upungungufu wa mvua katika maeneo haya  na kwa hali hii katika miezi hiyo inatarjiwa kupungua kwa matukio ya vimbunga na hivyo kusababisha mvua chache katika msimu wa vuli.

Amewashauri wakulima kuandaa mashamba na pembejeo mapema pamoja kuzingatia ushauri wa maafisa ugani wa kilimo kwa matumizi sahihi ya ardhi na mbegu  na kutumia kwa uangalifu na kuhifadhi akiba ya chakula walio nayo na wakulima katika maeneo hayo kuvuna mifugo ikiwa katika hali nzuri ya kiafya na wakulima kuzalisha na kuhifadhi malisho ya kutosha ili itumeke katika kipindi cha upungufu wa mvua.

Kijazi amezishauri mamlaka za miji kuchukua hatua za kuhakikisha kuwa mifumo na njia za kupitisha maji zinafanya kazi katika kiwango cha kutosha ili kuepusha maji kutuama na kupelekea mafuriko  na uharibifu wa miundombinu.

No comments:

Powered by Blogger.