LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAUZO SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM YAPANDA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Na James Salvatory BMG Dar
Idadi ya mauzo katika soko la hisa Dar es salaam (DSE), imepanda mara mbili na kutoka bilioni 3.8 hadi kufikia bilioni tisa huku idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa zikiwa zimepanda kwa asilimia 49 kutoka shilingi 724,000 hadi milioni moja.

Akizungumza jana na waandishi wa habari Jijini dar es salaam, Meneja biashara na mauzo, Meryy Kinabo, alisema kampuni tatu zinazoongoza kwa idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa ni TBL kwa asilimia 54%,SWISS  kwa asilimia 16%  Na CRDB kwa asilimia 11%.

Aidha alisema kuwa ukubwa wa mtaji wa soko umepanda kwa 2.48% kutoka 20.8 trilioni kufika 21.3 trillioni  huku ukubwa wa mtaji wa makampuni ya ndani umebaki kwenye kiwango kile kile cha panda 8.2 Trillion.

Kinabo aliongeza sekta ya viwanda (IA) wiki hii imeshuka kwa pointi 2.62 baada ya bei za hisa za TBL kushuka kwa 0.08% Sekta ya huduma za kibenki na kifedha (BI) wiki hii imepanda kwa pointi 3.38 baada ya bei kupanda kwenye kaunta za DSE kwa 12.04%, sekta ya huduma za kibiashara (CS) wiki hii iko vilvile baada ya bei za hisa za Swissport kubaki TZS 3,543.02

No comments:

Powered by Blogger.