LIVE STREAM ADS

Header Ads

MRATIBU WA MPIRA WA KIKAPU MKOANI MWANZA APANIA KURUDISHA HESHIMA YA MCHEZO HUO.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Displaying _DSC2503.JPG
Judith Ferdinand, Mwanza
Mratibu wa mchezo wa mpira wa  kikapu (basketball) mkoa wa Mwanza, Bahati Kizito (kushoto), amepania  kurudisha heshima ya mchezo huo kuanzia mkoa,kanda na taifa kwa ujumla.

Kizito aliyasema hayo jana,wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mafunzo ya kuwafundisha watoto kutoka shule mbalimbali mkoani hapa, yaliyoandaliwa na shirika la Planet Social Development ( PSD) kwa kushirikiana na Kocha George Ellis kutoka Marekani yalioitwa (Youth Basketball Clinic With Coach George Ellis from U.S.A), na kudhaminiwa na Pepsi,Moil na Mamb, yaliyofanyika uwanja wa CCM Kirumba.

Alisema kutokana na mchezo huo kutopewa kibaumbele kama  wa mpira wa miguu,wameamua  kufundisha watoto , ili kuibua vipaji na kuendeleza mchezo wa mpira wa kikapu kama ilivyo nchi ya marekani.

Pia alisema, baada ya kuwapatia mafunzo hayo, kabla ya mwaka huu kuisha, wataanzisha ligi ya  mpira wa kikapu katika shule sambamba  kuwa na viwanja vingi kwa ajili ya mchezo huo na kuhakikisha kocha waliopo wanawajibika ipasavyo.

Hata hivyo aliwaomba wazazi na wadhamini mbalimbali kujitokeza kuunga mkono mchezo huo kwa kuwanunulia vifaa,ili kuendeleza vipaji na kukuza mchezo huo.

Kwa upande wake Ellis alisema, serikali ya Tanzania pamoja na Chama cha Taifa cha Mpira wa Kikapu ( TBF) wanatakiwa kuunga mkono juhudi zinazoonyeshwa na mratibu huyo,sambamba na wadhamini kujitokeza kudhamini, kwani Marekani inafanya vizuri katika mikoa mchezo huo kutokana na kupata wadhamini wengi.

Naye Mratibu wa Jr MBA Bahati Mgunda alisema,wameamua kumualika George kuwafundisha watoto wadogo mbinu za kucheza mpira wa kikapu na stadi za maisha,ili kusaidia kuinua vipaji na kuhamasisha watoto hao kupenda mchezo huo.

Vilevile alisema ili kuendeleza vipaji na kukuza mchezo huo wataanzisha ligi ya taifa itakakuwa inafanyika mwishoni mwa mwaka na kutumia siku chache kwa watoto waliochini ya umri wa miaka 17.

Hata hivyo mchezaji wa taifa wa mpira Wa kikapu  Murshid Mudricat aliwaomba wazazi kuwasaidia na kuwa acha watoto wao washiriki katika mchezo huo ili waweze kuonyesha vipaji walivyo navyo.
Displaying IMG_3595.JPG

No comments:

Powered by Blogger.