LIVE STREAM ADS

Header Ads

MEYA WA MANISPAA YA KINONDONI JIJINI DAR ES SALAAM AOMBA KUONANA NA RAIS MAGUFULI JAPO KWA DAKIKA TATU.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Displaying 2.jpg
Msitahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniphace Jacob, akionesha raman ya majengo ya Magomeni Kota.

Na James Salvatory, BMG Dar
Mara baada ya siku mbili kupita tangu rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzan, Dkt.John pombe Magufuli, kutatua swala la wakazi wa Magomeni Kota kwa kuwaahidi kuwajengea nyumba nyingine na kuwapangisha bure kwa miaka mitano mara baada ya ujenzi kumalizika, naye Meya wa manispaa ya kinondoni, Boniphance jacobo, amemuomba rais kuonana nae hata kwa dakika tatu,  kwa lengo la kumueleza ukweli kuhusu namna  mradi wa magomeno kota ulivyoshindwa kutekelezwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini dar es salaam, meya huyo alisema ameshangazwa na viongozi wa  serikali akiwemo mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya ya kinondoni pamoja na waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, Willium Lukuvi, ambao walikuwa na mkutano wa kiserikali karibu na ofisi yake ila hawakumpa mwaliko ambapo hata hivyo aliamua kuhudhuria.

Baada ya kwenda kwenye mkutano huo hakupewa hata dakika moja kuweza kuongea mbele ya rais japo alikuwa akihusishwa kwa kiasi kikubwa na kumuomba  rais kuweza kuonana kwani ana jambo la kutaka kumuambia  kuhusu waziri wake wa ardhi maendeleo na makazi.

No comments:

Powered by Blogger.