LIVE STREAM ADS

Header Ads

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI MKOANI DAR ES SALAAM ATAKA WAKWEPA KODI KUTOONEWA HURUMA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Displaying IMG-20160902-WA0031.jpg
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Ally Salum Hapi (kulia) akipewa maelekezo na Meneja wa Mamlaka ya Mapato kimkoa, Kinondoni, Wallace Mnkande (kushoto) wakati mkuu huyo wa wilaya alipofanya ziara ya kushitukiza katika mamlaka hiyo jana.
Na James Salvatory - BMG Dar
Displaying IMG-20160902-WA0030.jpg
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es salaam, Ally Salum Hapi, amemuagiza Meneja wa Mamlaka ya Mapato kimkoa wa Kinondoni, Wallace Mnkande, kutowaonea huruma wale wasiolipa kodi kwani huduma zote muhimu za kijamii ikiwemo elimu bure na huduma za  Afya zinaendeshwa kwa kodi.

Akizungungumza jana jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kushtukiza katika Mamlaka hiyo, Hapi alisema Manispaa ya Kinondoni ina wafanyabiashara wakubwa na walipa kodi wengi hivyo kila mtu akitimiza wajibu wake ipasavyo mamlaka hiyo itaweza kuvuka kiwango cha kukusanya kodi.

Aidha alisisitiza kwamba Serikali kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato itahakikisha wakazi wa Kinondoni wanalipa kodi, pia katika hatua nyingine amemtaka meneja huyo kuboresha mfumo wa kutoa huduma kwa walipa kodi na kuhakikisha wanawapa elimu kuhusu masuala ya kodi.

Meneja wa Mamlaka hiyo, Wallace Mnkande, alisema changamoto kubwa ni pale wanapokwenda kukutana na walipa kodi ambapo hukuta wahusika wakiwa hawapo katika maeneo yao ambapo kwa sasa wamekuwa wakitoa taarifa kwa wahusika  lini watakwenda na muhusika hutakiwa kudhibitisha kama atakuwepo.
Displaying IMG-20160902-WA0029.jpg

No comments:

Powered by Blogger.