MWANZA WAFIKIWA NA HUDUMA ZA WAKALA WA USAJILI WA BIASHARA NA LESENI NCHINI BRELA.
Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Na Annastazia Maginga, Mwanza.
Katika kuhakikisha serikali ya awamu ya tano inakuza uchumi kupitia viwanda, wakala wa usajili wa biashara na leseni (Brela) imefungua tawi jipya mkoani Mwanza kwa ajili ya usajili wa makapuni na viwanda.
Kufuataia uwepo huo wa Brela, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, aliwataka wafanyabiashara kurasimisha biashara zao kufuatia uwepo wa wakala wa usajili na leseni (Brela) Mkoani hapa.
Akizungumza na wafanyabiashara hao juzi jijini Mwanza kwenye semina ya uhamasishaji juu ya majukumu ya Brela, Mongella alisema huduma za kurasimisha biashara itakuwa rahisi kupatikana kutokana na kwamba awali ilikuwa shida kwani huduma hiyo ilikuwa ikitolewa jijini Dar-es-salaam.
"Wadau watumie fursa hii vizuri ya kusajili biashara ili kurasimisha biashara zao na tufaidike na Brela kuwepo hapa"alisema Mongella.
Aidha kwa upande wake Afisa mtendaji Mkuu wakala wa usajili wa biashara na leseni (Brela), Frank Kanyusi, alisema makapuni 10 jijini Mwanza yametuma maombi ya usajili baada ya kutoa semina ya uhamasishaji hapo Jana.
Makapuni hayo yamethibitika jana ambapo yalifanyiwa usajili papo kwa hapo ikiwa fursa pekee kwa wakazi wa jiji la Mwanza baada ya wakala kufungua ofisi ya huduma hiyo kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Akizungumza na waandishi wa habari Jana Afisa mtendaji Mkuu wa Brela Frank kanyusi alisema kuwa huduma inahitaji kuwafikia wananchi ili kufahamu urasimishaji wa biashara ili kufikia uchumi wa viwanda.
"Mpaka sasa Mwanza makapuni yaliyothibitisha ni 10 japo bado tutaendelea kupokea maombi kwa sababu tupo kwa ajili ya jukumu hilo na gharama za kufungua kampuni kwa mtaji unaoanzia 20,000 hadi shilingi milioni moja ni elfu 95,000 lakini pia kupunguza gharama za mtu kufuata usajili Dar-es-salaam"alieleza Kanyusi.
Aidha alieleza kuwa walifanikiwa kufungua huduma hiyo kwa njia ya mtandao ambapo usajili wake ni shilingi 20,000 na kwamba tangu mwaka Jana hadi sasa wamefanikiwa kusajili makapuni elfu 80.
"Tangu tuanze usajili wa makapuni hadi hivi sasa yako laki moja na elfu hamsini lakini kwa mwaka jana makapuni yalikuwa elfu tisa na viwanda ni 20"alisema Kanyusi.

No comments: