BAA MAARUFU JIJINI MWANZA THE CLIMAX YATOA TUZO KWA WAFANYAKAZI WAKE
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, Amiri Mkalipa kampuni ya The Climax inayotoa huduma ya chakula, vinywaji na burudani jijini Mwanza, kwa kutambua mchango wa wafanyakazi wake na kuwaandalia hafla ya pongezi iliyoambatana na kuwakabidhi tuzo maalum.
Pia Mkalipa amesema kampuni hiyo imekuwa mstari wa mbele kurejesha kwa jamii faida inayopatikana akitolea mfano namna ilivyosaidia watoto wenye mahitaji maalumu wakati wa tamasha la Good Morning Rock City ambapo msanii Mboso ametumbuza kwa mara ya pili jijini Mwanza, eneo la Rock City Mall ilipo The Climax.
Mkalipa aliyasema hayo Jumatatu Februari 09, 2026 wakati akizungumza kwenye hafla ya Usiku wa Tuzo za The Climax Staff Awards iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mambo Leo Beach wilayani Ilemela na kutumia fursa hiyo kutoa rai kwa wawekezaji wengine kuiga mfano huo bora.
Naye Mkurugenzi wa The Climax, Charles Marick alisema kuthamini mchango wa wafanyakazi kunasaidia kuimarisha umoja na mshikamano katika kushirikiana kufanya kazi kwa bidii. Pia alisema ni muhimu kurejesha kwa jamii sehemu ya faida inayopatikana kwani jamii ndiyo inawezesha biashara kufanyika.
Kwa upande wake Mratibu wa hafla hiyo, Baraka Nyororo alisema uwepo wa matamasha mbalimbali jijini Mwanza unasaidia kuimarisha uchumi hivyo ataendelea kutumia ubunifu kwa kushirikiana na wawekezaji ili kufanikisha kwa ubora zaidi matamasha hayo.
Baadhi ya wafanyakazi wa The Climax walitoa shukurani kwa uongozi kwa kutambua mchango wao na kuahidi kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo na matarajio ya kampuni katika kuwahudumia wananchi.
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Amir Mkalipa.
Mkurugenzi wa The Climax, Charles Marick.
Mkurugenzi wa The Climax, Charles Marick (kushoto) akikabidhi tuzo kwa wafanyakazi wake.
Watoto wakifurahia chakula kilichoandaliwa na The Climax kwa ajili yao.
Tazama Video hapa chini





No comments: