LIVE STREAM ADS

Header Ads

MWENYEKITI WA CCM MKOANI MWANZA AFUNGUA MILANGO KWA WAPINZANI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Judith Ferdinand, Mwanza
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza, Dkt.Anthony Diallo (kushoto), amefungua milango na kuwakaribisha watu wanaotaka kujiunga na chama hicho,wakiwemo makada wa  vyama vingine vya siasa.

Kauli hiyo aliitoa juzi wakati wa hafla ya kumkabidhi kadi ya CCM, John Nzwalile aliyekuwa Katibu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Mwanza aliyejiunga na chama hicho, na kudai  viongozi wake, wanawachochea vijana kumpinga Rais Dkt.John Magufuli jinsi anavyoendesha nchi.

"Kwa kuwa Nzwalile hakuwahi kuwa mwanachama wa CCM na alikuwa kiongozi  wa ngazi ya mkoa CHADEMA, hivyo ameamua kujihudhuru mwenyewa hatuna budi kumpokea na kumkaribisha, ili aweze kuwa mwanachama atakayewezesha kuongeza mbinu za ushindi katika chaguzi zijazo za serikali za mitaa," alisema Diallo.

 Aidha aliongeza kuwa,CCM iko tayari kuwapokea wale wanaotaka  kuwa wanachama wa chama hicho kutokana na misingi yake ya kudumisha amani na umoja, kujikita kuhamasisha maendeleo ya nchi na kutetea wananchi walio wanyonge.

Naye  Nzwalile alisema, baada ya juzi  kujivua kwenye  chama cha  CHADEMA watu wamezoza sana ila hatoweza kujibu vifaranga     bali walioatamia na kutotao, kwani uamuzi ni wake kwa ajili ya maslahi ya taifa.

“kuwa mpinzani  siyo kabila kusema kwamba hauwezi kubadilisha ,mnyonge mnyongeni haki yake mpeni kwa nini  ni ng'ang'anie  kukaa CHADEMA wakati  ninaona yale yote tuliokuwa tunapigia kelele  kwa  serikali,  Rais Magufuli ameyafanyia kazi kwa matendo kwa muda mfupi, hivyo  sina haja ya kukaa huko," alisema Nzwalule.
Picha zaidi Bonyeza HAPA.

No comments:

Powered by Blogger.