LIVE STREAM ADS

Header Ads

USIYOYAJUA KUHUSU KUPATWA KWA JUA 2016.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Image result for kupatwa kwa juaDunia hii leo imeshuhudia tukio la kihistoria la kupatwa kwa jua ambapo tukio hilo limeonekana kwa uzuri zaidi katika wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.

Watu mbalimbali wakiwemo wageni kutoka mataifa mbalimbali wamesafiri hadi Rujewa,wilayani Mbarali kushuhudia tukio hilo lililoanza saa 4:17 asubuhi hadi Saa 7:56 adhuhuri.

Mbali na Mbarali maeneo mengine ambayo yameshuhudia kupatwa kwa jua kikamilifu ni Katavi, Ruvuma hadi Masasi ambapo tukio jingine kubwa la kupatwa kwa jua kama hili litatokea miaka 15 ijayo ambapo kwa mara ya mwisho kupatwa kwa jua kulitokea mwaka 1977.

Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla, na mwenzake wa mkoa mpya wa Songwe, Chiku Gallawa, walikuwa ni miongoni mwa watu waliojitokeza kushuhudia tukio hilo.


Kitalaamu kuna aina nne za kupatwa kwa jua ambapo miongoni mwa hizo ni kupatwa kabisa ambapo jua lapotea kabisa kwa dakika chache. Hali hii huonekana kwenye kanda nyembamba duniani kinapopita kitovu cha kivuli. kupatwa kipete; mwezi huonekana mdogo kuloko jua. 

Kwa hiyo duara ya kung'aa ya jua ni kubwa kuliko duara ya mwezi na mwanga wa jua waonekana kama pete na kupatwa kwa jua kisehemu ambapo katika eneo kubwa la kivuli cha kando watu huona upungufu wa mwanga; kiasi chake hutegemea umbali na kitovu cha kivuli. 
Na BMG kwa msaada wa Mtandao.

No comments:

Powered by Blogger.