WAAJIRI WATAKIWA KUFIKISHA MICHANGO YA WAAJIRIWA WAO KWA WAKATI.
Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na James Salvatory Bmg-Dar
Mamlaka ya Usimamizi na udhibiti wa sekta ya hifadhi ya Jamii (SSRA) imewataka waajiri wote nchini kuhakikisha wanapeleka fedha za mchango kwa wakati ili kuepusha ucheleweshwaji wa kupata mafao kwa mwajiriwa mara baada ya kustaafu.
Mkuu wa Mahusiano na uhamasishaji wa SSRA Sarah Kibonde amesema hayo alipokuwa akizungumza na wanahabari wakati wa semina ya Mfuko wa hifadhi ya jamii.
Aidha Sarah amebainisha kuwa ni vyema kwa mwajiri kumuachia Uhuru mtumishi wake kuchagua mfuko anaoutaka kujiunga badala ya kampuni kuwachagulia watumishi wake mifuko ya hifadhi, kwani kufanya hivyo kunamnyima mwanachama haki yake ya msingi ya kuchagua mfuko anaohitaji.
Naye mkurugenzi wa Sheria kutoka SSRA Onorius Njole ameeleza kuwa endapo mwajiri atachelewesha mchango wa mwajiriwa wake kwenye mfuko wa hifadhi atatozwa tozo ya asilimia 5% lakini pia ataweza kupelekwa mahakamani, ndani ya mwezi mmoja baada ya makato na pia SSRA kuweza kumfungulia kesi ya madai ya mchango.
Akizungumzia juu ya fao la kujitoa Njole amefafanua kuwa SSRA kwa kushirikiana na Serikali wanadhamiria kuleta fao mbadala litakalo mlinda mwanachama baadaya kupoteza ajira yake.

Kujua Zaidi Bonyeza HAPA
No comments: