LIVE STREAM ADS

Header Ads

WANANCHI ILEMELA WATAKIWA KUTUMIA FURSA ZILIZOPO KWA AJILI YA MAENDELEO YAO.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Judith Ferdinand, Mwanza
Wananchi wa Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, wametakiwa kutumia fursa zilizopo kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi sambamba na kuleta maendeleo binafsi,kata,wilaya, mkoa na taifa kwa ujumla.

Wito huo jana na Katibu wa Mbunge wa Jimbo  la Ilemela, Heri James, aliyemwakilisha Mbunge Angelina Mabula, katika kongamano la wajasiriamali liliondaliwa na Wenyeviti wa mitaa ya Nyamanoro Mashariki Trasisius Kabuche na Mkudi Salum Salum lililofanyika katika uwanja wa mnara wa vodacom Kata ya Nyamanoro mkoani hapa.

James alisema, wilaya hiyo  inafursa nyingi hasa kata ya Nyamanoro lakini anashangaa wananchi wake hawataki kutumia na badala yake wanaishia kulalamikia serikali kuhusu ajira.

Pia alisema,  umefikia wakati wa wananchi kuchangamkia fursa zilizopo ambazo zitakuwa chachu ya kutatua changamoto ya ajira na kujiinua kiuchumi, kwa kuunda na kusajili vikundi  ili kupatiwa fedha na serikali za kuendeleza miradi watakayokuwa nayo.

Vilevile aliwaomba vijana kushirikiana pamoja  kubuni na kuzitumia  fursa katika suala la maendeleo, na kuacha tabia ya ubinafsi hali inayopelekea kushindwa na kukata tamaa.
Aidha aliwaomba viongozi wa serikali za mitaa kushirikiana na jamii kutambua na kutumia fursa zilizopo, ili kuleta maendeleo.

Kwa upande wake Kabuche  aliwaomba wananchi wa kata ya Nyamanoro kutumia fursa ya soko la Rocky City Mall kwa utengenezaji wa bidhaa mbalimbali kama vikapu pamoja na kufanya shughuli nyingine za ujasiriamali.

Naye  Salum aliiomba jamii ya kata hiyo kuacha majungu na mambo ya ovyo,badala yake wajitokeze  kuchangamkia fursa zinazojitokeza kwa ustawi wa maendeleo binafsi, mtaa na Taifa kwa ujumla.

Mmoja wa washiriki wa kongamano hilo Anes Alexander alisema, jamii ikijikita katika ujasiriamali na kutumia fursa zilizopo ,taifa litaondokana na suala la ukosefu wa ajira.

No comments:

Powered by Blogger.