LIVE STREAM ADS

Header Ads

WENGI WAJITOKEZA KUPIMA AFYA ZAO KATIKA VIWANJA VYA MMNAZI MMOJA JIJNI DAR ES SALAAM.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto) akizungumza wikendi iliyopita na Wananchi waliofika katika viwanja vya Mnazi Mmoja kupata vipimo na kupatiwa ushauri na Madaktari kutoka Hospitali Mbalimbali Jijini Dar es Salaam.
Picha na Khamis Mussa
Wananchi wakiwa na watoto wao katika viwanja vya Mnazi Mmoja
Wananchi wakiwa katika mistari ambao hawajapata namba
Mkuu wa Idara ya magonjwa ya dharura na Ajali Hospitali ya Taifa Muhimbili Dk. Juma Mfinanga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa Zoezi la kupima vipimo kwa wananchi bure lililo ratibiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kwa kushirikiana na Madaktari kutoka Hospitali mbalimbali za Dar es Salaam ikiwemo, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aga Khan Hospital, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ikiongonzwa na Rais wa Chama cha Madaktari Figo Tanzania na pia ni  Daktari Bingwa wa Figo Dk. Onesmo Kisanga 
  Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Grece (kushoto) Magembe akiwaonyesha jambo wananchi walio jitokeza kupata huduma ya vipimo  kutoka kwa Madaktari wa Hospitali mbalimbali ikiwemo Hospitali ya Taifa Muhimbili mkoa wa Dar es Salaam ilioratibiwa na Ofisi ya  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda lililofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini humo na kutokana na mwitikio wa wananchi huwenda ziku zitaongezwa baada ya Mkuu huyo kujadiliana na madaktari hao ambapo Septemba 25 hapo awali ilikuwa ndio siku ya kuhitimisha zoezi hilo.
Wafanyakazi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa  wa Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja
Zuhura Shaba (54) akiwa amebebwa na baadhi ya Madaktari na wafanyakazi wa Afya baada ya kujikuta amepoteza fahamu mara baada ya kufika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam , baada ya muda na mpiga picha hizi alibahatika kuongea nae na kuanza kusema kwa utaratibu kinacho msumbua.

Baada ya kumdadisi alisema, yeye ni Mtoto wa 7 na  baba yake ezi za uhai wake miaka ya nyuma  aliwahi shika nyadhifa mbalimbali Serikalini kama, Waziri wa Afya, Meneja Mkonge Tanga, aliwahi kuwa Mbunge, hivyo anamshukuru Mkuu wa Mkoa na Mungu amuongoze kwa kila anachokifanya kwa Jamii ya Kitanzania na kumshukuru Rais wa Tanzania kwa kumpa maono ya kumteua, Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.

Ameishukuru timu nzima ya Madaktari kwa moyo wao kuona jamii ya kitanzani bado ina hali duni na kushirikiana na Mkuu wa Mkoa kutuletea zoezi hili, nashukuru baada ya kujikuta napoteza fahamu nimejikuta nipo katika chumba huduma ya haraka na kupata huduma na sasa najiona ninanafuu.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bi Sophia Mjema (kushoto) akishiriki zoezi la kugawa namba kwa wananchi walioitikia wito wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Baadhi ya Wananchi wakiwa wamenyoosha mikono wakitarajia kupata namba kwa ajili ya kupatiwa huduma ya vipimo

Askari Polisi akizungumza na baadhi ya Wananchi waliojitokeza katika viwanja vya Mnazi Mmoja
Joice Mgeta akipatiwa vipimo na Dk. Danieli Chacha (kushoto) mara baada kujikuta anaishiwa nguvu ghafla akiwa katika foleni ya kusubiri kupata namba , kulia ni  Mkuu wa Idara ya magonjwa ya Dharura na Ajali Hospitali ya Taifa Muhimbili Dk. Juma Mfinanga

No comments:

Powered by Blogger.