LIVE STREAM ADS

Header Ads

JICHO LA BMG: KASI YA UJENZI WA MAKAZI HOLELA MILIMANI KATIKA JIJI LA MWANZA NA ATHARI ZAKE.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Serikali kupitia kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Willium Lukuvi, imetangaza zoezi la kurasimisha makazi yaliyojengwa kiholela katika maeneo ambayo yalikuwa hayajapimwa na kutoa hati ya umiliki kwa wamiliki wa makazi hayo ili waweze kutambulika na kuzitumia hati hizo katika taasisi za kifedha kupata mikopo kwa ajili ya shughuli zao.

Hata hivyo zoezi hilo halitawahusu wakazi walio kwenye maeneo hatarishi ikiwemo mabondeni, milimani na hifadhi za barabara na tayari mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba, amepiga marufuku ujenzi katika maeneo hayo kuendelea.

Pichani ni makazi yaliyojengwa kiholela katika moja ya maeneo hatarishi (milimani) eneo la Mabatini Jijini Mwanza na unaambiwa miaka ya 1980 hakukuwa na nyumba hata moja katika eneo hilo hivyo serikali ilipuuzia kasi ya ujenzi katika maeneo ya aina hiyo na sasa madhara yake yamekuwa makubwa ikiwemo vifo kutokana na baadhi ya nyumba kuporomokewa na mawe pamoja na utiririshaji wa vinyesi wakati wa mvua na hivyo kusababisha magongwa ya miripuko ikiwemo kipindupindu.
JICHO LA BMG

No comments:

Powered by Blogger.