LIVE STREAM ADS

Header Ads

KAMPUNI YA MAGAZETI YA NEW HABARI CORPORATION YALALAMIKIWA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

 Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam, John Kayombo (Kushoto), akiwa na Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ubungo Dkt.Mariam Malliwadh baada ya kuwasili katika kampuni ya New Habari Corparation alikofanya ziara ya kushtukiza jana.
Na Mathias Canal
Kelele ziosizo za kawaida huenda zikawasababishia wafanyakazi wa Kampuni ya New Habari Corparation matatizo ya kutosikia kutokana na kutokuwa na vifaa madhubuti vya kuzuia kelele hizo.

Hayo yalibainika jana wakati wa Ziara ya ghafla iliyofanywa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Mhe John L. Kayombo ambapo miongoni mwa mambo yaliyobainika ni pamoja na kelele hizo zisizo za kawaida ambazo zinazotolewa na mtambo wa kutengeneza magazeti katika kampuni hiyo ambazo zinahatarisha uwezo wa wafanyakazi wa kusikia .

Ziara ya Mkurugenzi Kayombo ya kutembelea katika kampuni hiyo imekukuja muda mfupi baada ya kusikia vilio vya wananchi na wafanyabiashara wanaoishi jirani na kiwanda hicho.

Baada ya malalamiko ya wananchi kumfikia, Mkurugenzi Kayombo akaenda New Habari House bila kutoa taarifa kwa uongozi wa kiwanda kwa nia ya kuona hali halisi.

Akiwa kiwandani hapo Mkurugenzi Kayombo alikagua maeneo mbalimbali yanayozunguka kiwanda na hatimaye akafika kwenye mashine inayochapisha magazeti yanayotolewa na kampuni hiyo.

Mashine hiyo ilikuwa inapiga kelele hali ambayo sio rahisi kwa binadamu kukaa eneo hilo lakini alikuta wafanyakazi wakiwa hapo tena bila kifaa chochote cha kuzuia au kupunguza sauti hizo.

'' Hili jambo sio zuri haiwezekani mashine ipige kelele kiasi hiki huku wafanyakazi wakiendelea kuzalisha magazeti,huu ni ukatili na ni kwenda kinyume na haki za binadamu"alisema Kayombo.

No comments:

Powered by Blogger.