LIVE STREAM ADS

Header Ads

KAMPUNI YA UWEKEZAJI NCHINI YA UTT YAANZISHA HUDUMA YA USIMAMIZI WA MALI NA RASILIMALI KWA WATEJA WAKE.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Displaying mkurugezi w  masokona uhusiano utt.JPGNa James Salvatory BMG-Dar
Kampuni ya uwekezaji nchini UTT, imeanzisha huduma ya usimamizi wa mali na rasilimali  ijulikanayo kama Wealth Management itakaowezesha watanzania kujenga utaratibu wa kuwekeza fedha zao  katika taasisi za kifedha badala ya kuhifadhi pesa majumbani na sehemu nyingine ambayo haziwaletei faida yoyote.

Akizungumza jana na wandishi wa habari jijini Dar es salaam, Mkurugezi wa masoko na uhusiano UTT, Daudi Mbaga, alisema kuwa huduma hii itamsaidia   mteja kuwekeza fedha zake mahali     salama na baadae kunufaika kutokana na faida ya uwekezaji itakayopatikana kwa kipindi husika

Mbaga alisema  huduma hiyo ni tofauti na huduma zingine za kuweka hisa kwani yenyewe huzalisha kuanzia asilimia 10% na kuendelea na amewakaribisha watu wote wenye nia ya kutumia
huduma hiyo kufika jengo la Sukari house ghorofa ya pili ili waanze kufurahia Huduma hiyo.  

Aliongeza  kuwa uwazishaji wa huduma ya usimamizi wa mali utasaidia taifa kufikia matarajio wa uchumi wa kati na maendeo  kama  watanzania watajikita kwenye sekta ya uwekezaji wenye faida huku akiwataka watanzania kutambua nafasi ya uwekezaji wa faida na kuachana na dhana ya kuhifandhi pesa  majumbani au sehemu ambayo pesa haizalishi faida.

No comments:

Powered by Blogger.