LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAADHIMISHO YA SIKU YA POSTA DUNIANI 2016, MKOA WA MWANZA WANG'ARA KWENYE SHINDANO LA UANDISHI WA BARUA KITAIFA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Meneja wa Shirika la Posta mkoani Mwanza, Julius Chifungo, akizunguza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani ambayo kimkoa yamefanyika leo katika Shule ya Saint Mary's Seminary (Nyegezi Sekondari) Jijini Mwanza.

Siku ya Posta duniani huadhimishwa ifikapo Oktoba 09 kila Mwaka ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu ya Siku ya kuanzishwa kwa Umoja wa Posta Duniani ulioanzishwa mwaka 1874 katika mji wa Berne nchini Switzerland ukijumuisha mataifa 192 duniani.
Na BMG

Maadhimisho hayo yamekwenda sambamba na zoezi la kukabidhi zawadi kwa Washindi wa Uandishi wa barua Kitaifa kutoka mkoani Mwanza ambapo washindi watano kati ya 10 bora kitaifa wametoka Saint Mary's Seminary (Nyegezi Sekondari) Jijini Mwanza.

Washindi hao na nambari walizoshika kwenye mabano ni, Denis Bahati Stephen (01), Samwel Lufungulo Somelo (02), Vitalis Aloo Awasi (03), Kizito Eliakimu Paschal (04) na Fredrick Elias Mayunga (08).

Washindi wa Tano na Sita wametoka Shule ya Mazinde Juu mkoani Tanga, Mshindi wa Saba ametoka Shule ya Lugalo mkoani Iringa, huku Washindi wa Tisa na 10 pia wakitoka Shule ya Mazinde Juu mkoani Tanga.

Meneja wa Posta mkoani Mwanza, Julius Chifungo amesema shindano la uandishi wa barua huwashirikisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wasiozidi umri wa miaka 15 ambapo shule za msingi lugha ya kiswahili na kiingereza hutumika na kiingereza pekee kwa shule za sekondari. 

Amebainisha kwamba wanafunzi huandika barua yenye mane kati ya 500 na 1,000 kulingana na mada iliyotolewa na kwamba mwaka huu mada ilikuwa ni "Jiandikie barua ukiwa na miaka 45" ambapo barua ya mshindi wa kwanza itakwenda kushindanishwa na barua za washindi wengine kutoka nchi 191 wanachama wa Umoja wa Posta Duniani ambapo mshindi wa kwanza nchini ataliwakilisha taifa kwenye shindalo hilo nchini Switzerland.
Katibu Mtendaji wa Idara ya Elimu, Jimbo Kuu la Mwanza, Alex Masasi, ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo akizungumza ambapo amewahimiza wanafunzi kuongeza bidii katika masomo yao hususani kuwa bora kwenye kusoma, kuandika na kuzungumza lugha nyingi tofauti na kiswahili na kiingereza.
Wanafunzi wakimsikiliza kwa umakini Katibu Mtendaji wa Idara ya Elimu, Jimbo Kuu la Mwanza, Alex Masasi, ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho Siku ya Posta yaliyofanyika leo Jijini Mwanza.
Mkuu wa Shule ya Saint Mary's (Nyegezi Sekondari) Jijini Mwanza, akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani. Siku ya Posta duniani hufanyika kila mwaka Oktoba 08, hivyo yamefanyika leo Oktoba 07 kutokana na ratiba ilivyopangwa.
Mshindi wa Nane Kitaifa kwenye Mashindano ya Uandishi wa barua, Fredrick Elias Mayunga kutoka Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza akipokea zawadi yake.

Mshindi wa Nane amepokea Cheti cha utambuzi, Tisheti, Kamusi ya Kiingereza, begi la kubebea daftari, Kikokoteo pamoja na fedha Elfu Arobaini (40,000).
Mshindi wa Nne Kitaifa kwenye Mashindano ya Uandishi wa barua, Kizito Eliakimu Paschal, kutoka Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza akipokea zawadi yake.


Mshindi wa Nne amepokea Cheti cha utambuzi, Tisheti, Kamusi ya Kiingereza, begi la kubebea daftari, Kikokoteo pamoja na fedha Laki Moja na Elfu Ishirini (120,000).

Mshindi wa tatu Kitaifa kwenye Mashindano ya Uandishi wa barua, Vitalis Aloo Awasi, kutoka Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza akipokea zawadi yake.


Mshindi wa Tatu amepokea Cheti cha utambuzi, Tisheti, Kamusi ya Kiingereza, begi la kubebea daftari, Kikokoteo pamoja na fedha Laki Mbili (200,000)

Mshindi wa Pili Kitaifa kwenye Mashindano ya Uandishi wa barua, Samweli Lufungulo Somelo, kutoka Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza akipokea zawadi yake.


Mshindi wa Pili amepokea Cheti cha utambuzi, Tisheti, Kamusi ya Kiingereza, begi la kubebea daftari, Kikokoteo pamoja na fedha Laki Tatu (300,000)

Mshindi wa Kwanza Kitaifa kwenye Mashindano ya Uandishi wa barua, Denis Bahati Stephen, kutoka Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza akipokea zawadi yake.


Mshindi wa kwanza amepokea Cheti cha utambuzi, Tisheti, Kamusi ya Kiingereza, begi la kubebea daftari, Kikokoteo pamoja na fedha Laki Nne (400,000)

Mkuu wa Shule ya Saint Mary's Seminary, Maximillian Buluma, akipokea zawadi ya shule hiyo baada ya kuwa shule iliyotoa washindi kitaifa pamoja na washiriki wengi. Amepokea mpira pamoja na Cheti kutoka Shirika la Posta.
Kulia ni Meneja wa Posta Mwanza, Julius Chifungo, akimkabidhi mgeni rasmi zawadi
Washindi wa shindano la kuandika barua nchini, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Shirika la Posta Mwanza, Waalimu wa Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza, Mgeni Rasmi pamoja na Wazazi.
Washindi wa shindano la kuandika barua nchini kutoka shule ya Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza wakiwa kwenye picha ya pamoja na Wazazi wao.
Washindi wa shindano la kuandika barua nchini, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Shirika la Posta Mwanza.
Washindi wa shindano la kuandika barua nchini, wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa shule ya Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza, Mgeni Rasmi pamoja na Meneja wa Posta Mwanza.
Washindi wa shindano la kuandika barua nchini kutoka shule ya Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza.
Washindi wa tatu bora katika shindano la kuandika barua nchini kutoka shule ya Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza
Afisa Masoko, Shirika la Posta mkoani Mwanza, Julius Mponda, akizungumza kwenye maadhimisho hayo
Mwalimu Victor Mgisha anayefundisha somo la Kiingereza shule ya Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza akizungumza kwenye Maadhimisho hayo.
Waalimu wa Shule ya Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza wakielezea furaha yao baada ya wanafunzi wa shule hiyo kuibuka washindi wa shindano la uandishi wa barua linaloandaliwa na Umoja wa Posta duniani na kufanyika kwa nchi wanachama 191 kote duniani.
Mwalimu wa Shule ya Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza, akisoma barua iliyompa ushindi, mshindi wa kwanza kwenye shindano la uandishi wa barua nchini.
Meneja wa Shirika la Posta mkoani Mwanza, Julius Chifungo, akizunguza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani ambayo kimkoa yamefanyika leo katika Shule ya Saint Mary's Seminary (Nyegezi Sekondari) Jijini Mwanza.
Mshindi wa kwanza Kitaifa kwenye shindano ya uandishi wa barua, Denis Bahati Stephen, kutoka Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza akizunguza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani ambayo kimkoa yamefanyika leo katika Shule ya Saint Mary's Seminary (Nyegezi Sekondari) Jijini Mwanza.
 Mshindi wa pili Kitaifa katika shindano ya uandishi wa barua, Samweli Lufungulo Somelo, kutoka Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza akizunguza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani ambayo kimkoa yamefanyika leo katika Shule ya Saint Mary's Seminary (Nyegezi Sekondari) Jijini Mwanza.
Bonyeza HAPA Kutazama Mwanza walivyoibuka kidedea kwenye Shindano la Uandishi wa barua mwaka 2015 Kitaifa.

No comments:

Powered by Blogger.