LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAMLAKA YA MAPATO NCHINI TRA YAENDELEA KUFANYA VYEMA KWENYE UKUSANYAJI WA MAPATO.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Tangazo Muhimu

Na James Salvatory,BMG Dar
Katika kuhakikisha lengo la kukusanya kodi ya shilingi trioni 15.1  kwa mwaka 2016/17 linatimia, Mamlaka ya mapato Tanzania TRA imeendelea kufanya vizuri na imeweza kukusanya jumla ya shilingi trilioni 3.59  katika kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo wa mwaka wa fedha.

Akizumza na wandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Mkurungenzi huduma na elimu kwa mlipa kodi kutoka Mamlaka hiyo, Richard Kayombo, amesema makusanyo hayo yanajumuisha mwezi Julai, shilingi trioni 1.05, mwezi Agost trioni 1.13  na September shilingi trioni 1.37.

Aidha amesema kuwa ukusanyaji wa mapato ya serikali unaenda sambamba na kuelimisha wananchi kuhusu wajibu wao wa kulipa kodi sahihi  na kwa wakati.

Katika hatua nyingine TRA imewakumbusha wakazi wa dar  es salaam kuwa zimebaki siku tisa kumalizia zoezi la uhakiki na uboreshashaji wa taarifa za namba ya utambulisho wa mlipakodi (TIN) kwa mikoa ya dar es salaam na Zanzibar ,tayari mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) imehakiki na kutoa vyeti vipya vya TIN 15,467.

Aidha Kayombo, amewahimiza wasafirishaji wa mizigo ya kwenda mikoani kudai risiti za EFD's pindi wanaponunua bidhaa na kuwa nazo wakati wanaposafirisha mizingo ili kuepuka usumbufu huku wafanyabiashara wakihimizwea kutoa risiti kwa wateja wao ili kuhakikisha makusanyo ya yanakusanywa kwa uhakika .

No comments:

Powered by Blogger.