LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAPUMZIKO YANAVYOATHIRI MAUZO KWENYE SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na James Salvatory, BMG Dar
Kuwepo kwa mapumziko marefu ya wiki  ikiwa ni pamoja na kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Julius Nyerere imelezwa kuwa chanzo kikuu cha mauzo ya hisa kushuka kwa asilimia 91 kwa wiki hii katika Soko la hisa la Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa Habari jana jijini Dar es salaam, Afisa Mwandamizi wa Soko la hilo Mary Kinabo  amesema kutokana na mapumziko marefu ya mwisho wa wiki yalioyoambatana na maadhimisho ya kumbukumbu ya Kifo cha hayati  baba wa taifa Mwalimu nyerere yameshachangia kushuka
kwa mauzo yahisa sokoni hapo kutoka bilioni 32.5 hadi kufikia bilioni 3 kwa wiki hii.

Amesema Wakati hali hii ikitokea  moja kwamoja mauzo  yameshuka hadi kufikia bilioni 3  kutoka bilioni 32.5 wakati kampuni zinazo ongoza kwamauzo ni pamoja na CRDB (53%)
ikifuatiwa kampuni ya TCC (41%) wakati TBL Ikishika nafasi ya tatu kwa mauzo kwa asilimia (4%).

“wakati Benki ya Crdb ikiongoza kwa mauzo katika Soko hilo ukubwa mtaji wa wasoko umeshuka kwa asilimia tatu kutoka trioni 21.49 hadi trioni20.8 huku mtaji wamakampuni ya ndani ukibakikatika kiwango cha awali ,”alisema kinabo

No comments:

Powered by Blogger.