LIVE STREAM ADS

Header Ads

MPAMBANO WA SIMBA NA YANGA ULIKUWA ZAIDI YA MECHI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Mchezo ligi kuu ya Tanzania bara baina wapinzani wa soka la Tanzania, Simba na Yanga, ulikuwa zaidi ya mchezo, baada ya kuwakutanisha wapinzani wa kisiasa nchini, Mwigulu Nchemba (CCM) na Freeman Mbowe (Chadema) jukwaa moja.

BMG imeshuhudia viongozi hao wakishangilia pamoja wakati Yanga ilipopata goli la kwanza, ambapo Nchemba ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi alikuwa amevalia jezi ya Tanzania, alionekana kushangilia zaidi na kwa furaha goli hilo huku pembeni akiungwa mkono na Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema aliyekuwa amevalia magwanda ya chama chake.

Hii imetoa tafsiri kwamba, siasa si uadui, siasa si ugomvi na kwamba michezi ni kiunganishi pekee kinachoweza kuwaunganisha watu ama kundi lenye itikadi tofauti katika maisha.

Hadi kipyenga cha mwisho, timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1 ambapo Yanga imekuwa ya kwanza kupachika bao lililofungwa na Amis Tambwe dakika ya 26 kipindi cha kwanza huku Simba ikisawazisha bao hilo kupitia kwa Shiza Kichuya aliyepiga kona ya moja kwa moja, dakika ya 87 kipindi cha pili.

Awali mchezo huo uliopigwa kwenye simba la taifa Jijini Dar es salaam, ulisimama kwa muda baada ya kutokea fujo iliyohusisha mashabiki wanaodaiwa kuwa ni wa Simba waliokuwa wakipinga bao la Yanga, huku viti uwanjani hapo viking'olewa ambapo polisi wa kutuliza ghasia wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kutuliza hali.

No comments:

Powered by Blogger.