LIVE STREAM ADS

Header Ads

MKURUGENZI WA JIJI LA MWANZA AWATAKA WATENDAJI MITAA NA KATA KUTIMIZA WAJIBU WAO.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Judith Ferdinand, Mwanza
Watendaji wa Kata na Mitaa iliyopo ndani ya halmashauri ya Jiji la Mwanza, wameagizwa kutimiza wajibu wao kwa kusimamia sheria sambamba kuhimiza wananchi kutunza na kufanya usafi wa mazingira.

Agizo hilo limetolewa  jana na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Kiomoni Kibamba, wakati akizungumza na watendaji hao katika kikao  kilichofanyika ukumbi wa Gandh Hall mkoani hapa.

Kibamba alisema, hali ya usafi wa jiji hilo hauridhishi,hivyo ni jukumu la viongozi wa mitaa kuhimiza wananchi kufanya usafi na kutunza mazingira.

Pia alisema, watendaji hao wanatakiwa kutimiza wajibu wao na kusimamia sheria kwa kutatua changamoto zinazojitokeza katika maeneo yao na kuacha kukaa ofisini wakisubili mishahara inayotokana na kodi za watu maskini.

Hata hivyo aliwataka, wananchi kufuata  na kuzingatia kanuni za afya, kujenga na kutumia vyoo bora sambamba na kuacha kutiririsha maji machafu katika mitaro,ili kuepuka magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu.

Kwa upande wake  Ofisa Mahusiano wa Jiji hilo Elirehema Kaaya aliwataka, wananchi kubadili tabia zao kwa kutunza mazingira ili kurudisha hadhi  ya jiji hilo ya  kuongoza kwa usafi nchini na kuwa bora Afrika Mashariki.

Vile vile alisema, watendaji kata na mtaa wajibu wao ni kuhamasisha jamii kufanya usafi kwani atakayebainika anachafua mazingira faini ni sh 50000 au kufikishwa mahakamani.

Naye  Ofisa Mtendaji wa Kata ya Nyamagana Thereza Mtesigwa aliwaomba wananchi kuchukulia suala la usafi ni la kila mmoja, hivyo kushirikiana na viongozi kutekeleza.

Aidha Ofisa Mtendaji wa Kata ya Nyegezi  Charles Musso alisema, wananchi hawapo tayari katika suala la usafi hivyo kata yake inawaelimisha na kuwahamasisha juu ya usafi, pamoja na kuanza kufanya ukaguzi wa nyumba kwa nyumba na wayakayemubaini anachafua mazingira na kuririsha maji machafu watampiga faini ya sh 50000.

No comments:

Powered by Blogger.