LIVE STREAM ADS

Header Ads

MKUU WA WILAYA YA KAHAMA AWATAKA WANANCHI KUTUMIA BARABARA KAMA CHANZO CHA MAENDELEO.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na Shaban Njia. Kahama
WANANCHI  Mkoani shinyanga wametakiwa kutumia barabara kama chanzo na kichocheo  kikuu kwa kuleta  maendeleo Mkoani humo  badala ya kutumia kama chanzo cha  kusababisha ulemavu wa maisha kwa wananchi.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu aliyasema hayo katika uzinduzi wa Wiki ya nenda kwa kusalama barabarani ambayo kimkoa ilifanyika  katika Wilaya ya Kahama.

Nkurlu alisema kuwa kwa sasa ni muhimu kwa Wananchi utumia barabara kama chanzo kikuu cha maendeleo katika maeneo hayo badala ya kutumia kama chanzo kikuu cha kusababishi watu ulemavu wa maisha nap engine vifo.

Mkuu huyo wa Wilaya ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika uzinduzi huo wa wiki ya nenda kwa usalama Mkoani Shinyanga alisema kuwa utumiaji wa barabara kama kichocheo cha maendeleo kunaweza kusababisha mabadiliko makubwa ya kiuchumi hasa kwa utumiaji wa miundombinu ya kama hiyo ya barabara.

Pia Mkuu huyo wa Wilaya aliwataka Waendesha Pikipiki maarufu kama Bodaboda kufuata sheria za barabarani ili ili kupunguza ajali ambazo sio za lazima zinazotokana na uzembe unaosababishwa na watumiaji wa vyombo hivyo vya moto.

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu aliwataka bodaboba hao kujifunza kwa makini kuhusu matumizi sahihi ya barabara ikiwa sambamba na kupata elimu sahihi kuhusu sheria za usalama barabarani  hali ambayo itaweza kuwasaidia katika kupunguza ajali.

Hata hivyo Mkuu huyo wa Wilaya hakusita kuwaagiza Askari wa usalama barabarani kuwa wakali na kuwafikisha katika vyombo vya sheria wale wote ambao watakuwa wakivunja sheria za usalama barabarani hali ambayo itakuwa ni mfano kwa wale wote wenye tabia kama hizo.

Wiki ya nenda kwa usalama barabarani yenye kauli mbiu ya hatutaki ajali tunataka kuishi salama, imeadhimishwa kimkoa katika Wilaya ya Kahama huku ikishirikisha baadhi ya makundi ya Waendesha Baiskeli, pikipki, mabasi ya abiria pamoja na watuaji wengine wa vyombo vya moto.

No comments:

Powered by Blogger.