LIVE STREAM ADS

Header Ads

MKUU WA WILAYA YA NYANG'WALE MKOANI GEITA ATAKA KAMPUNI YA ACACCIA KUDUMISHA AMANI NA WANANCHI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na Shabani Njia, Kahama
Katika kile kinacho wagharimu Wawekezaji wengi na wananchi katika maeneo mbali mbali yaliyowekezwa kuwa na migogoro ni hali ya kuwepo kwa mahusiano duni miongoni mwa makundi hayo mawili.

Mkuu wa Wilaya ya Nyang’wale Mkoani Geita,Hamimu Gwiyama,ameutaka uongozi wa mgodi wa Dhahabu Bulyanhulu,ulioko katika halmashauri ya Msalala wilayani Kahama Mkoani Shinyanga, kuendelea kudumisha mahusiano kwa wananchi wa vijiji 14 vinavyozunguka mgodi huo.

Hayo aliyasema juzi wakati alipozungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama Fadhil Nkurlu, aliyepaswa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha Mahusiano Sports Bonanza yaliyofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Kakola Kata ya Bulyanhulu katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama.

Kwa upande wake Afisa Mahusiano wa Acacia Bulyanhulu Sala Ezra Terry alisema bonanza hilo lilikuwa na lengo la kudumisha mahusiano baina ya Wananchi na mgodi huo ambapo hali hiyo itafanya mgodi utekeleze shughuli za maendeleo kwa wananchi pamoja na kufanya shughuli za uwekezaji ziwe za ufanisi zaidi.

Bonanza hilo liliandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Seach for
Comon Ground linalofanya shughuli zake ndani ya mgodi wa Bulyanhulu ambapo bonanza hilo limefadhiliwa na kampuni ya Acacia.

No comments:

Powered by Blogger.