LIVE STREAM ADS

Header Ads

Naibu Waziri wa Afya afanya ziara katika Hospitali ya Wilaya ya Iramba mkoani Singida na kutoa maelekezo muhimu.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
dsc_0559
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Iramba namna wanavyokusanya mapato.
Na Andrew Chale

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya Iramba Mkoani Singida na kukagua huduma za Afya katika Hospitali ya Wilaya pamoja na Zahanati ya Kisimba ndani ya Wilaya hiyo.

Katika ziara hiyo, Dk. Kigwangalla ameweza kubaini mapungufu mbalimbali ambayo ameagiza yapatiwe ufumbuzi ndani ya miezi mitatu.

Akiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Iramba, ameweza kujionea huduma mbalimbali zitolewazo Hospitalini hapo hata hivyo ameagiza uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha wanafunga mfumo wa ukusanyaji mapato wa malipo wa kisasa kwa njia ya kielektroniki.

“Mfumo wa malipo ya kielektroniki umeleta ukombozi mkubwa sana kwenye mahospitali nchini. Mapato yameongezeka. Udhibiti wa mapato umekuwa rahisi. Nawaagiza nanyi Hospitali ya Iramba kuhakikisha munafunga mfumo huu wa malipo wa kisasa hususani kwenye: Maabara,Chumba cha upasuaji (Theatre), Dirisha la dawa, na sehemu zote zenye kuingiza mapato”. Ameeleza Dk.Kigwangalla wakati wa kutoa maagizo hayo.

Katika Zahanati ya Kisimba ambayo ipo umbali wa zaidi ya Kilometa 10, Dk.Kigwangalla ameweza kujionea huduma mbalimbali kwenye Zahanati hiyo ambayo ni mpya huku ikiwa msaada mkubwa kwa wananchi wa vijiji hivyo.
dsc_0584

No comments:

Powered by Blogger.