LIVE STREAM ADS

Header Ads

Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla afunga rasmi kongamano la 30 la Wanasayansi Watafiti.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
dsc_0653
Na Andrew Chale
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla, jana amefunga rasmi Kongamano la 30 la Kimataifa la Wanasayansi Watafiti lililoandaliwa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) lililokuwa la siku tatu Jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri Dk. Kigwangalla aliwaeleza wanasayansi hao watafiti kuwa Serikali inashirikiana nao bega kwa bega katika jukumu la maendeleo hapa nchini hivyo  uwepo wao ni kielelezo tosha cha maendeleo ya Taifa na watu wake hasa katika Nyanja za kiuchumi, Afya, Mazingira na mambo mengine  ya kimaendeleo.

Aidha, alibainisha kuwa changamoto za magonjwa ya virusi yanayotokana na Mbu ambapo ameahidi amewahidi wanasayansi hao na Wizara yake kushirikiana nao katika kulipitia ufumbuzi.

Dk.Kigwangalla aliwahakikishia Wanasayansi hao  kuwa, masuala yote ya kuimalisha huduma za Maabara katika ngazi za msingi kwani suala hilo amekuwa akilifanya kila mahala anapokwenda kwenye ziara zake juu ya upatikanaji wa huduma  Maabara bora kwenye sehemu za Afya.

“Nimependa maombi yenu haya juu ya kuimalisha huduma za Maabara kwenye ngazi za msingi. Suala hili nimekua nikilifuatilia kila ziara zangu kwenye vituo vya Afya na Hospitali zote hivyo nitalibeba hili na nitaendelea nalo kwa sababu nina aamini kutoa huduma za afya bila kuwa na huduma madhubuti za Maabara ni kuchezea afya za watanzania wenzetu, Ni lazima tuwe na huduma bora za Maabra zetu na suala hili tutakaa mimi na Mh. Waziri kuona namna ya kufanyia maboresho zaidi.” Amesema Dk.Kigwangalla.

Aidha,  Dk. Kigwangalla aliwatunukia vyeti maalum wanasayansi  Vijana walioshiriki kwenye kongamano hilo.

Kongamano  hilo  la siku tatu, Oktoba 4-6, awali lilizinduliwa na Makamu wa Rais Mh. Mama Samia Suluhu Hassan ambaye pia aliwahakikishia Wanasayansi Watafiti hao  kuwa Serikali inatambua mchango wao na wataendelea na juhudi za kuwalinda kwani ni nguzo muhimu ya kufikia malengo ya millennia ya ukuaji wa kiuchumi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Dk. Mwele Malecela amesema kufikia tamati ya kongamano hilo ni ishara tosha maandalizi yake yalikuwa mazuri na washiriki wote walioshiriki wamejifunza mengi  huku wakiwa ni mfano wa kuigwa kwa elimu walioipata hapo.

Nchi  mbalimbali za Afrika, Ulaya na Amerika ambapo  washiriki zaidi ya 300 wameshiriki  huku mada zaidi ya 220 zikiwasilisishwa na kujadiliwa kwa pamoja na wataalam hao.

Nchi ambazo zinashiriki kongamano hilo kuwa ni Afrika Kusini, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Uganda, Australia, Denmark, Ubeljiji, Uholanzi, Uingereza, Ujerumani, Uswis, Kanada, Sweden, Norway, Marekani, Bangladesh, Thailand na wenyeji Tanzania.
dsc_0670

No comments:

Powered by Blogger.