LIVE STREAM ADS

Header Ads

TAASISI YA MIRADI NA MAENDELEO YA MIUNDOMBINU YACHANGIA MAAFA YA TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KAGERA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.comdsc_0722
Msajili wa Hazina Ndugu Lawrence Mafuru akipokea mfano wa Hundi kutoka kwa wakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa UTT – Projects Ndugu Uli Mtebe  na Afisa Masoko wa UTT Projects Bi. Kilave Atenaka kiasi cha shilingi milioni kumi kwa niaba ya Kamati ya Maafa Bukoba chini ya ofisi ya Waziri Mkuu.
Na Andrew Chale

Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundo Mbinu iliyo chini ya Wizara ya Fedha,(UTT-PID) imetoa kiasi cha Shilingi Milioni Kumi kwa ajili ya kuchangia maafa ya tetemeko la ardhi lililotokea Bukoba Mkoani  Kagera hivi karibuni.

Tukio hilo la kukabidhi fedha hizo zilizowakilishwa kwa njia ya mfano wa hundi limefanyika leo Oktoba 7.2016, katika ofisi za Msajili wa Hazina Jijini Dar es Salaam kwa Msajili wa Hazina.

Awali akipokea ujumbe uliomwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo ya UTT-PID, Msajili wa Hazina Ndugu Lawrence Mafuru ameshukuru UTT-PID kwa wito wao huo wa kuchangia maafa kwa kuwakumbuka wananchi hao ambao wengi wao wanahitaji msaada mkubwa.

Naye  Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa UTT –PID, Ndugu Uli Mtebe alimweleza Msajili huyo wa Hazina kuwa, Taasisi yao imekuwa karibu na watu wa Kagera-Bukoba kwani licha ya kufanya miradi, pia wamekuwa karibu na jamii hiyo kwa kuwachangia mambo ya kimaendeleo ikiwemo elimu na miundombinu.
dsc_0725
Msajili wa Hazina Ndugu Lawrence Mafuru akipokea mfano wa Hundi kutoka kwa mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa UTT – Projects Ndugu Uli Mtebe kiasi cha shilingi milioni kumi kwa niaba ya Kamati ya Maafa Bukoba chini ya ofisi ya Waziri Mkuu. Kulia ni Afisa Masoko wa UTT Projects Bi. Kilave Atenaka.

No comments:

Powered by Blogger.