LIVE STREAM ADS

Header Ads

SHIRIKI LA KUTETEA HAZI ZA WASICHANA NA WANAWAKE KIVULINI LATAKA WANAJAMII KUCHUKUA HATUA DHIDI YA UKATILI WA KIJINSIA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Judith Ferdinand, Mwanza
Kutokana na kuendelea kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wasichana na wanawake nchini  huku watu wakishuhudia na kuyanyamazia, jamii imetakiwa kujenga muitikio wa pamoja wa kuchukua hatua dhidi ya ukatili wa aina zote.

Shirika la Kivulini linalojihusisha na utetezi wa haki za wanawake na wasichana, limeamua kuanzisha kampeni ya kitaifa inayoitwa "Tunaweza" inayolenga kuhamasisha wanamabadiliko 150,000 wa mkoa huu, wajitokeze hadharani kupinga na kuukata ukatili bila kujali lawama,vitisho,  hawatonyamaza pamoja na kuchukua hatua.

Akiongea jana kwenye mdaharo wa walimu na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Pamba iliyopo wilayani Nyamagana, mkoani hapa, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Yassin Ally, alisema kampeni hiyo inashirikisha jamii, shule, taasisi zinazotakiwa kusimamia haki na sheria kama jeshi la polisi na mahakama, ili kujenga muitikio wa pamoja wa kuukataa ukatili na kuchukuliwa hatua.

"Shida iliyopo ni watu kuunyamazia ukatili, tunataka tufanye watu wajitokeze hadharani bila kujali lawama, vitisho wawe wanamabadiliko ambao hawataunyamazia ukatili na watachukua hatua dhidi ya ukatili wa aina zote, wanaotendewa watoto wa kike na wanawake, tunataka tujenge muitikio wa pamoja wa kuukataa ukatili na kuchukua hatua kwa sababu imeonekana matendo mengi yanayotokea yanashuhudiwa na watu lakini wanayanyamazia," alisema Ally.

Aliongeza kuwa, kwa mujibu wa takwimu za taasisi ya takwimu ya Taifa ya mwaka 2010, imeonekana kuwa asilimia 56 ya watu walioko kwenye ndoa wanatendeana ukatili ambapo kati ya familia 10, sita zina mahusiano yenye ukatili.

Hata hivyo alisema, watoto wanapokuwa kwenye familia hiyo inaathiri mahudhurio, ufaulu na umakini wake katika masomo na kupelekea kujihusisha katika mashinikizo rika kama kupata mimba za utotoni, kuacha shule au kujiingiza kwenye makundi yanayotumia dawa za kulevya.

Akiongea kwa niaba ya wanafunzi waliohudhuria mdaharo huo, Msafiri Juma, alililiomba shirika hilo kuanzisha klabu kwa shule za msingi na sekondari, ili wanapofanyiwa ukatili wajue wapi pa kuripotia matendo hayo na kupata msaada.

Naye  mmoja wa walimu wa shule hiyo, Rahel John, alisema wanafunzi wapewe nafasi ya kusikilizwa kutokana na baadhi ya walimu kuwatendea matendo ya ukatili kama kuwachapa viboko na kuvuliwa nguo wanapokuwa shuleni.

No comments:

Powered by Blogger.