LIVE STREAM ADS

Header Ads

Taasisi ya miradi na maendeeo ya miundombinu UTT-PID yaendesha semina kwa Wahariri wa vyombo vya habari na wadau wake Dar es salaam.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

5Mgeni rasmi katika semina hiyo, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na Maendeleo, Bw. Juston Lyamuya akifungua rasmi semina hiyo ya Wahariri wa Vyombo vya Habari pamoja na Wadau wa UTT-PID katika semina ya ushirikishaji wa wadau katika kuboresha miundombinu, uliofanyika ukumbi wa mikutano wa Julius nyerere jijini Dar es salaam jana Oktoba 19.2016.
Na Andrew Chale
4 8 6Mkurugezi wa Manispaa ya Lindi Jomary Satura akitoa semina kuhusu fursa za uwekezaji zinazopatikana katika manispaa hiyo wakati wa mkutano wa jukwaa la wahariri lililoandaliwa na Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundombinu (UTT-PID).
dsc_2204
dsc_2151dsc_2187 dsc_2154Mhariri wa Michuzi Media Group, (MMG) ambaye pia ni mmiliki wa blog ya JIACHIE (Michuzijr) Ahmad Michuzi JR, akichangia mada katika semina hiyo
dsc_2153Baadhi ya Wahariri wakichangia mada katika semina hiyo
dsc_2198 dsc_2168 dsc_2210 dsc_2211 dsc_2226 dsc_2220 dsc_2218 dsc_2212
11
3Baadhi ya wadau pamoja na Wahariri wa vyombo vya habari wakifuatilia semina hiyo
2Mkurugezi mkuu wa UTT-PID Gration Kamugisha akifunga semina hiyo kwa Wahariri wa vyombo vya habari (Hawapo pichani) na wadau wa mbalimbali katika semina ya ushirikishaji wa wadau katika kuboresha miundombinu, uliofanyika ukumbi wa mikutano wa Julius nyerere jijini Dar es salaam jana Oktoba 19.2016.
10Mkurugezi mkuu wa UTT-PID Gration Kamugisha kushoto akiagana na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na Maendeleo Juston Lyamuya ambaye alikuwa mgeni rasmi katika semina ya ushirikishaji wa wadau katika kuboresha miundombinu, uliofanyika ukumbi wa mikutano wa Julius nyerere jijini Dar es salaam Oktoba 19.2016.
*************************
Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundombinu (UTT-PID), imekutana na Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini pamoja na wadau katika kuboresha miundombinu, semina iliyofanyika mapema jana Oktoba 19 katika ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

Semina hiyo iliyofunguliwa na mgeni rasmi Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na Maendeleo, Bw. Juston Lyamuya aliipongeza UTT-PID kwa namna ilivyoweza kubobresha miundombinu pamoja na shughuli za kimaendeleo hususani katika upatikanaji wa viwanja na hati kwa wananchi kwenye miradi yake mbalimbali hapa nchini.

“Sote kwa pamoja tunaipongeza UTT-PID, kwa namna inavyoendesha shughuli zake hasa katika sehemu mbalimbali za Halmashauri, Miji na Manispaa kwani zimeboresha miundombinu na hta wananchi kufaidika na miradi hii ambayo ipo kwa uwazi sambamba na kuendeshwa kisasa” amesema Mgeni rasmi huyo.
Katika semina hiyo, mada mbalimbali zimewasilishwa na wadau ikiwemo miradi ya upamaji ardhi, miundombinu, ujenzi na fursa zilizopo katika maeneo ya Majiji, Miji na Halmashauri hapa nchini.

Aidha, Manispaa ya Lindi ilipongezwa kwa namna ya kipekee kufikia malengo katika miradi yake na UTT-PID Kwani ubia wao huo umekuwa wa mafanikio makubwa.

Naye Mkurugezi wa Manispaa ya Lindi Jomary Satura wakati wa kuwasilisha mada katika semina hiyo juu ya fursa za uwekezaji zinazopatikana katika manispaa hiyo, amewaomba wananchi na wadau kujitokeza kwa wingi Manispaa ya Lindi ilikunufaika zaidi na fursa zilizopo.

No comments:

Powered by Blogger.