LIVE STREAM ADS

Header Ads

TAASISI ZA ELIMU ZA KANISA LA EAGT LUMALA MPYA JIJINI MWANZA ZATOA MWANGA KWA WATOTO, WADAU WAKARIBISHWA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com


Na George Binagi-GB Pazzo
Wadau wa elimu nchini wamehimizwa kutoa ushirikiano wao ili kuhakikisha kwamba watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi hawakosi haki yao ya msingi ya kupata elimu.

Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza, Daniel Kulola (kushoto), ametoa rai hiyo wakati akizungumza na Lake Fm kuhusiana huduma za kielimu zinazotolewa na kanisa hilo kupitia taasisi zake za EAGT Student Centre pamoja na Development Dreams Attainment Foundation.

Amesema bado kuna idadi kubwa ya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi na ambao wazazi na walezi wao hawana uwezo wa kuwahudumia mahitaji ya shule ikiwemo mavazi, hivyo ni vyema wadau wa elimu wakiwemo wanajamii wenyewe wakajitoa ili kuwasaidia watoto hao.

Zaidi ya watoto 270 wanaotoka katika familia zisizojimudu kiuchumi na waliokuwa wanaishi katika mazingira hatarishi katika Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, wamenufaika na taasisi za kanisa la EAGT Lumala Mpya hususani kupata fursa ya kwenda shule.

No comments:

Powered by Blogger.