LIVE STREAM ADS

Header Ads

WANANCHI KAHAMA WAOMBA TAKUKURU KUINGILIA KATI UGAWAJI WA FEDHA ZA TASAF.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na Shaban Njia
Siku chache baada ya serikali ya awamu ya tano kutoa tamko la walioshiriki katika ufujaji wa fedha za wananchi za Mfuko wa maendelo ya jamii (TASAF) kwamba watachukuliwa hatua watendaji wote walioshiriki katika zoezi hilo,wananchi katika halmashauri ya wilaya Kahama mkoani Shinyanga, wameomba TAKUKURU kufanya uhakiki sahihi kubaini zoezi liliendeshwa hususani Vijijini.

Katika kikao cha Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Kahama kilichufanyika juzi mjini hapa,wananchi kupitia wawakilishi wao,wameitaka Taasisi ya kuzua na kupamba na Rushwa (TAKUKURU) kufika maeno ya Vijijini kuhakikisha kama zoezi hilo lilifanyika kwa usahihi.

Juzi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki aliagiza  Tasaf kuhakikisha inafuatilia kaya zote ambazo zilizoingizwa katika mpango huo bila kuwa na sifa zinazostahili, kwa kuziorodhesha kwa majina, wanapoishi na kiasi cha fedha walichopokea.

Wakiongea katika Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Kahama baadhi ya Madiwani  walisema kuwa fedha hizo za Tasaf III, katika Halmashauri ya Mji wa Kahama hazikufika katika kaya zilizolengwa badala yake walipewa watu wenye uwezo ambao kimsingi hawakustahili kupata fedha hizo.

Mmoja wa Madiwani hao ambaye ni Diwani wa kata ya Nyahanga Michael Magire alisema kuwa suala la ugawaji wa fedha katika baadhi ya Vijiji halikufanyika kama ilivyotarajia hali ambayo iliacha malalamiko makubwa kwa baadhi ya kaya masikini.

Diwani huyo alisemakuwa kuhusu fedha hizo Wananchi amekuwa wakiibiwa sana fedha zao na kupewa watu ambao hawakustahili kufaidika na fedha hizo hivyo kusababisha waliostahili kupata kulalamika.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi hao alisema kuwa fedha hizo ziliozotolewa na TASAF kunauwekano mkubwa kuwa hazikufika katika kaya husika ambazo ni masikini na hivyo kupewa kaya ambazo zilikuwa zikiweza katika maisha na hivyo kusababisha mizozo kwa kaya zilizostahili.

Akijibu hoja kuhusu hoja hiyo  Afisa wa TAKUKURU katika mkoa maalumu wa Kahama, Chrisantus Ndibaiukao alisema kuwa,changamoto inayoipata taasisi yake ni pamoja na ushiriki wa wananchi  katika utoaji wa ushahidi pindi kesi zinapofikishwa mahakama.

Ndibaiukao alisema,kuna baadhi ya kesi ambazo zilishafikishwa mahakamani lakini changamoo kubwa inatokea pale Mashahidi wanapotakiwa kutoa ushahidi ndipo wanapokanusha ya kuwa wao hawausiki katika kesi hiyo kwani walilazishwa kutoa ushahadi.

Badhi ya Wananchi katika Halmashauri ya Mji wa Kahama wamekuwa wakilalamikia kuwa mgao huo uliokua ukitolewa na TASAF kuwa Maafisa hao wa Mfuko huo wa maendeleo ya jamii katika Halmashauri ya Mji wa Kahama haukweza  kuwafikia Wananchi walio masikini kama ilivyopangwa na hivyo kuiomba Taasisi hiyo ya kuzuia na kupamba na Rushwa Mkoa maalumu wa Kahama kufanya uchunguzi ili kubaini kama fedha hizo ziliwafikia walengwa wake.

Akijibu hoja juu ya kesi nyingi za TAKUKURU kushindwa mahakamani, alisema inatoakana na baadhi ya wananchi kushindwa kuthubutu kutoa ushirikiano wa dhati hususani ushahidi wa maelezo mbele ya mahakama na kesi nyingi kukosa ushshidi.

Pia alisikitishwa na baadhi ya wahusika pindi wanapofika mahakamani hukana maelezo yao ya awali mbele ya mahakama na kudai kuwa walilazimishwa kuandika au kueleza maelezo hayo licha ya kuwa baadhi ni viongozi wa dini hali ambayo husababisha mahakama kutupilia mbali mashauri mengi ya Taasisi.

Alisema hali hiyo imekuwa ni changamoto kubwa kwa jamii kubadilika na kuinga mkono TAKUKURU katika awamu ya tano kutoa ushirikiano ili kupamabana na vita dhidi ya rushwa .

Tangu januari mwaka huu jumla ya kesi tisa zilifikishwa TAKUKURU na Mahakamani ambapo 6 zishindwa huku 3 zikikatiwa rufaa kwa mamlaka ya juu kisheria.

No comments:

Powered by Blogger.